harieth kiliaki
Member
- Jun 30, 2015
- 18
- 15
Sijawahi kata tamaa katika maisha ya utafutaji.
Habari zenu wana jukwa hili.
Natumaini mnaendelea vizuri na Pole sana kwa wale ambao wanajisikia vibaya kiafya.
Jina la naitwa Neema Lusekelo.Ni mkazi wa jijini Dar es salaam. Nilizaliwa katika mkoa wa Arusha wilaya ya Monduli kata ya kosovo. Nilipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Mlimani iliyopo Monduli nilihitimu mwaka 2006. Nilichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Irkisongo ambapo nilihitimu kidato cha nne mwaka 2010. Nilifanikiwa na kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita mwaka 2013 katika shule ya Ruvu sekondari iliyopo Kibaha-Pwani. Nilifanikiwa kuchaguliwa kwenda kujiunga na masomo ya chuo kikuu 2013.
Nilifanikiwa kuchaguliwa kujiunga shahada ya kwanza katika chuo kikuu Cha Mlimani kilichopo jijini Dar es salaam na mwaka 2017 nilihitimu masomo hayo.
Harakati za kutafuta ajira zikaanza rasmi.Mwaka 2018 nilipata kazi katika kampuni fulani iliyopo wilaya ya Kinondoni Inayojihusisha na kuagiza magari kutoka Japan, nilifanya kazi kama afisa masoko. Mimi sikuwahi kusomea biashara kwahiyo nikama nilienda kupata ujuzi mpya. Nilifanya kazi miaka miwili, kazi mahali pale haikuwa nzuri au mbaya.
Malipo yalikuwa ya commission baada ya kuuza bidhaa ndipo utalipwa. Nilivumilia ile kazi kwani niliamini nifursa pekee ya mimi kunikutanisha na watu wengi ambapo naweza kutana na mtu mmoja atakayenisaidia kupata kazi ya ndoto yangu. Haikutokea vile nilivyofikiria ama kuwaza hatimaye baada ya muda huo niliacha ile kazi, kutokana cha sababu mbalimbali zilizojitokeza mahali pale zilizokuwa nje ya uwezo wangu.
Fedha nilizopata katika kazi hii nilifungua duka dogo.Biashara ya duka haikuniendea vizuri kabisa nilidumu mwaka mmoja nikalifunga baada yakuona mtaji unapungua.
Nikahamishia mtaji kwenye biashara ya pikipiki .Nilikuwa na nunua pikipiki mkononi mwa mtu(used).Nampatia kijana kwa makubaliano anatakiwa kuleta tsh 10,000 kila siku kwa muda tuliokubaliana na atakapomaliza itakuwa mali yake. Ashukuriwe Mungu biashara ilienda vizuri sana.
Hatimaye kijana alimaliza mkataba wake na kuchukua pikipiki nakuwa yakwake.
Nikachukua zile pesa na kununua pikipiki nyingine kwani biashara hii ilipendeza machoni mwangu Neema na nikaipenda kisawasawa laiti ningelijua!!!! Niliondoka na fundi kwenda kukagua hiyo pikipiki tukajiridhisha mimi na fundi wangu na kufanya malipo na hatimaye kuondoka na chombo chetu. Nikapata kijana alichukua na kuanza kufanya kazi,Ali fanya kazi kwa muda wa siku 20 tu.
Alifanikiwa kulipa pesa ya siku 10 tu na siku nyingine alishindwa na kuanza kutoa sababu ambazo zilimfanya ashindwe kuleta pesa kwa wakati na kazi ilimshinda na kuamua kurudisha pikipiki. Neema sikukata tamaa na kabisa nilitafuta kijana wapili. Alikuja na kukagua pikipiki ajiridhishwe na kusaini mkataba.
Majibu yake yaliuvunja moyo wangu sana. Alisema pikipiki ni mbovu sana asingeweza kuichukua. Niliamua nakuipeleka kwa rafiki yangu ambaye anautaalamu mkubwa juu ya hizi pikipiki, majibu yake yalikuwa mabaya zaidi kuliko ya yule kijana wa pili. Alikagua nakugundua tank la pikipiki lilikuwa limetoboka shokapu zimeisha nizakubadilisha, tairi la nyuma lakubadilisha pamoja na ringi lake. Gharama yake ilikuwa kubwa kiasi nisingeweza kumudu kwa muda ule.
Sikukata tamaa nikahamia kwenye biashara ya dagaa, Ninaye rafiki aliyeko Mwanza ajihushusha na biashara ya dagaa. Alinikutanisha na kaka mmoja ambaye yeye ni mvuvi kutoka kisiwa cha Bwiru ili anisaidie kupata dagaa moja kwa moja kutoka kisiwani.
Nilimtumia pesa yakuniletea dagaa, Siku niliyotarajia mzigo unatumwa nilipokea simu kutoka kwa mvuvi huyo kuwa dagaa wamekuwa adimu kwahiyo ameshindwa kunitumia mzigo.Nikasubiria siku,wiki na hatimaye mwezi umeisha bila yakupata taarifa za kuridhisha juu ya dagaa.
Nilivunjika sana moyo ,ukweli sikuwahi kupata dagaa mpaka Leo,niliamua kuachana na hii biashara baada yakuona inaniumiza moyo.Kilichobakia ananirudishia pesa nilizomtumia ameanza kurudisha kidogo kidogo na bado hajamaliza deni lake mpaka Leo.
Mwishoni mwaka 2021 ,nilikuwa kanisani katika maombi ,askofu alitangaza kuwa anaomba waumini wajitokeze kusaidia kazi ya ujenzi inayoendelea mahali pale.
Hakika nilijitokeza kwasababu wakati ule mimi sikuwa na kazi wala biashara yoyote, nikaona ni afadhali nikatumie muda huo kufanya kazi ya ujenzi kanisani. Kesho yake asubuhi na mapema sana niliwahi kufika kanisani. Nilikutana na fundi rangi na moja kwa moja nilianza kufundishwa namna ya kupaka rangi.
Nilijifunza kwa muda mrefu kidogo nikawa na mimi niko vizuri kiasi cha fundi mkuu kuniamini na kuweza kunipatia wanafunzi wengine wa kuwafundisha.
Hatimaye siku zilipita, Fundi mkuu alipata tenda Dodoma. Nilikuwa miongoni mwa aliowachagua kuambatana nae kwenda Dodoma. Wakati najifunza hii kazi nilipata changamoto sana kwani watu wanapopita nakuona mwanamke anafanya kazi ambazo zimezoeleka kuwa ni zawanaume basi huwa na mtizamo tofauti.
Pili, iliniwia vigumu kwa familia na ndugu wakaribu kunikubalia kufanya hii kazi kwanza nikutokana na elimu yangu pia afya yangu(kifua) haikuwa sawa kufanya kazi kama hii. Kwangu haikuwa tatizo sana ila nilichukua kama changamoto natakiwa kuishinda.
Naweza kusema hii kazi imeniletea faida sana ,kwani nimeweza kupata fedha zakujikimu ,kukulipa kodi na pia nimeweza kununua kiwanja maeneo ya kibaha. Nafurahi sana hii kazi imenifanya kwanza nijione watofauti na mwenye kipaji cha pekee.
Ingawa wakati mwingine napitia changamoto, kwani kuna mafundi ambao sio waadilifu tunapokuwa kwenye maeneo yakazi.Kwakuwa tayari ni mwanamke basi hukuchukulia kama anaweza kukufanya au kukuamrisha kufanya atakacho kwakuwa unahitaji wa hiyo kazi. Malengo yangu nikusimama mwenyewe na kufundisha wanawake wengi zaidi wenye uhitaji wakujisimamia kiuchumi.

Upvote
13