Sijawahi kuwasikia Millard Ayo au Maulid Kitenge wakiongea Kiingereza

Sijawahi kuwasikia Millard Ayo au Maulid Kitenge wakiongea Kiingereza

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
10,406
Reaction score
19,892
Hawa jamaa naona wana safari sana za kwenda nje, lakini sijawahi kuwasikia walau wakiongea hata sentence moja tu ya lugha ya kiingereza.

Mahojiano wanayoyafanya huko nje huwa ni wanawahoji Watanzania wenzetu tu na lugha inayotumika ni kiswahili kama kawaida.

Sasa nilitaka kujua huko nje kwenye safari zao wanazofanya, kwenye hotel au huduma nyingine za kijamii huwa kuna Wakalimani?
 
Nakazia...si tumekubaliana waandishi wa habari wa bongo Ni Kanjanjas' journalists.....
 
Cha muhimu Millard ni mbunifu sana na ana mkwanja mrefu hata wakongwe hao kina kitenge wanaiga kupitia kwake mambo ya online Tv ila wameshachelewa muhuni yuko mbali sana hategemei kuajiriwa tena yule
 
Hawa jamaa naona wana safari sana za kwenda nje, lakini sijawahi kuwasikia walau wakiongea hata sentence moja tu ya lugha ya kiingereza.

Mahojiano wanayoyafanya huko nje huwa ni wanawahoji Watanzania wenzetu tu na lugha inayotumika ni kiswahili kama kawaida.

Sasa nilitaka kujua huko nje kwenye safari zao wanazofanya, kwenye hotel au huduma nyingine za kijamii huwa kuna Wakalimani?
Badala ya kusifia mafanikio yao - bila kujali Elimu yao, wewe unauliza kama wanaongea lugha ya kigeni. Ukiongea Kiingereza vizuri kinakusaidi nini kama huna hela? Tuanze kujivunia vyetu!
 
Mkuu kwenye dunia ya maarifa lugha ni kitu kidogo sana. Yaani mbele ya watu walioelimika hiki unachoongea hapa ni ushamba mtupu. Wewe ni aina kamili ya watanzania tulio nao
Lugha ndio msingi wa maisha ya mwanadamu na maendeleo yake na ndio kitu cha kwanza kitakachotumika kati ya vita, amani na makubaliano.
Lugha ndio kitu cha kwanza ambacho unapaswa kuwa nacho ili kupokea maarifa kutoka sehemu yoyote ile duniani.

Hivyo lugha sio kitu kidogo hata kidogo.
 
La msingi kazi zao zinakwenda na wanachokusudia kukifanya ktk maisha yao wanakifanya. Na zaidi ya yote wanaingiza pesa, pengine zaid ya wanaojua kiingereza. Tuache kuwahusudu wakoloni.
 
Back
Top Bottom