Manchris Jbisd
JF-Expert Member
- Apr 9, 2013
- 691
- 494
Mimi ni mhitimu wa kidato cha sita mwaka huu. Baada ya kuwasikiliza waziri na wahusika wa Bodi ya mikopo kuhusu hili swala la ku-apply mkopo kabla ya matokeo, kijana wa watu nikawa mpole ukizingatia wao ndo wameshika mpini, nikajitosa nikaanza kufanya michakato hiyo. nikalipia m-pesa na nikapata ile transaction ID. tatizo ni pale napoingiza ID hiyo kwenye sehemu ya self-registration. nikiingiza wanasema haitambuliki ile ID yangu. wanasema nisubiri kama masaa mawili. mchakato huo niliufanya jana(tarehe 29). cha ajabu mpaka sasa hivi hawajaikubali. na pia mpaka sasa hivi simu zao za huduma zinaita tu bila kupokelewa, na wakati mwingine simu iko bize au haipatikani kabisa... sasa whats the rush wakati wao wenyewe hawapo makini na mitambo yao? i now dont know what to do anymore... yaan matokeo wanicheleweshee mimi, deadline nipewe mimi, afu mazinguzi wafanye wao... si ndo majanga haya!!!!