Asante mkuu, nashukuru Mungu kwa hilo🙏🙏Mkuu awali ya yote nikupongeze kwa utu ulouonesha kwa yule mtoto maana nafahamu ulimwangalia mtoto kwa jicho la kama mwanao
Swala la taarifa ilipaswa afanye hivyo maana ni uungwana kukujuza kinachoendelea.
Uzuri umekiri, yenda wema nenda zako. Hapo mkuu huna hatia hata mbele za Mwenyezi Mungu. Umetimiza agizo la mwenyezi Mungu [pendaneni]
Wanawake Kama hao Ni halali kutiwa na kuzalishwa na wababa tofauti tofauti na kutelekezwa imagine umeji sucrifice malipo yamekuwa Maumivu in short huyo anakuonea wivu..Habari za asubuhi wana JF,
Iko hivi, nina rafiki yangu ana mtoto (naweza nikasema ni single mom) ila isieleweke vibaya, nilisomaga nae O level huko ila nikama bahati tu tumejikuta tunaishi tena mtaa mmoja.
Ijumaa jioni wakati natoka tu ofisini alinipigia Simu akaniambia anashida kama naweza nipitie nyumbani kwao nikamuone, kwakua nilikua sina ratiba nyingine nikasema isiwe tabu kabla sijafika nyumbani nikapitia.
Nilimkuta yuko good ila mwanaye alikua anaumwa sana ile mtoto kazidiwa na akaniambia ameshindwa kwenda hospitali hana hela na almost kila aliyempigia simu wamemuahidi tu tangu asubuhi na hakuna aliyemtumia mpaka muda huo sa 1 jioni inaelekea saa 2.
Kiukweli sikua na hela and i was totally broke, yaani wiki ile iliyoisha mwenyewe nimeishi tu kwasababu nina wazazi maana nilikua nina mambo mengi yananihitaji hela kiasi kwamba sikua nimebakiwa na hata Mia mbovu. Lakini nikasema kwenye suala la kuokoa maisha ya mtoto isiwe kesi nikamwambia ngoja nirudi kwanza nyumbani, nikamsimulia mama tukaongea na dada yangu wakasema tu hapa kwa harakaharaka hatuna namna tumdanganye tu mzee kitu chochote jioni hii atupe hela, kweli mzee bila hiyana tukamshawishi akanipa 150k nikamfata kwao tukaenda hospitali usiku uleule.
Mtoto akapewa huduma ya kwanza na baadhi ya vipimo wakamlaza ili asubuhi aendelee na matibabu mengine (muda wote huo anawapigia ndugu zake wakiwemo na baba wa mtoto hata simu hawampokelei wengine), asubuhi yake niliomba tu ruhusa kazini nikawaambia nitachelewa ili nione mtoto atakua anaendeleaje.
Case ya mtoto ikawa kubwa wakasema tuende nae hospitali nyingine kubwa (Peramiho nadhani watu wa songea wanaijua), kuna vipimo alivyoambiwa wampime vilikua vinahitaji hela almost kama laki 2 tena nikamwambia mama akanitumia tukafanikisha. Kwasababu kazini nilikua wanapigapiga sana simu na nikaona wanaendelea vizuri na mama yake alikua ashafika nikamwambia naenda ofisini incase kimetokea chochote utatuambia nikampa na namba ya mama kama mimi nisipopokea ampigie, nikaondoka. The bad thing is nilikua busy busy sana hadi siku ikaisha sikuwatafuta tena.
Kinachoniumiza ni kwamba, jana mchana nilimpigia simu hakupokea nikaenda kwao sikukuta mtu, nikaenda hadi Peramiho tena kulivyo mbali nikaambiwa wameruhusiwa na hakunipa taarifa. Kuanzia jioni nimeingia WhatsApp naona ameweka status nyingi nyingi kufungua nikawa naona amescreenshot miamala yote ya watu waliokua wanamtuma hela na kuwapa credits Mungu awabariki sana kwa kuokoa maisha ya mwanae maana alikua kwenye hali mbaya sana na nini nini. Screenshot kama kumi hivi na kitu na amewataja na majina kabisa...
Cha ajabu hiyo miamala hakuna hata wa mtu mmoja uliofikia hata 30k, wote ni hizo hizo tu efu10 ef5 ef7, kawaandikia macaption mazito mazito. Nimebaki najiuliza mbona alikua ananiambia hawapokei simu, na hela inaonekana walimtumia siku ileile ambayo aliniambja na mimi niende kwake kumuona.
Mimi ambayo nilikua nae kuanzia siku ile hadi usiku nikaacha na kwenda kazini na tumeclear bills zote hata asante hajaniambia na wala taarifa kama wameruhusiwa hajanipa. Nimesubiri jana yote hadi leo saizi hajanipigia hata simu, Kina mama wananiuliza wanaendeaje nawaambia tu wanaendelea vizuri huku roho inauma.
Nimetenda wema nimeenda zangu wakuu, lakini bado roho inaniuma aisee😥😥
Hapana kushukulu ni hekima sana mbele za mungu iila huyu kazidi katoka pelamio ajamwambia mwenzie anampigia simu hapokei ndo dada wa watu imemuuma sana.Siku zote ishi kwa kusaidia bila kutegemea malipo yeyote. Iwe ya shukrani ama chochote.
Kwa sababu hata shukrani isingekuongezea chochote.
Amen 🙏🙏.. Huwezi amini nimefumba macho kweli na kuyasema hayo😃.. Barikiwa sana kiongoziNimekupenda bure!
That's true African woman should be like that! really touching aiseh!I appreciate it!!
Shukuru mtoto amepona TU!!Hilo jingine ni tatizo lake binafsi!!
Mara nyingi Huwa mnasumbuliwa na wivu na kisirani Cha wenyewe Kwa wenyewe!!
Anaweza his anakukomoa au unajidai una kazi na hela!kumbe ni wema wako tu!!
Kama una uchungu fumba macho mwambie Mungu nakushuru mtoto amepona!naomba unibariki TU Mimi na wazazi wangu!!
Yule mtoto ni WA mungu sio was kwake!!
Hapana, mtu mjinga ni lazima aambiwe kuhusu ujinga wake ili ajifunze na asije wafanyia wengine ujinga.Usimpigie, ataona una shida nae sana. Watu wa hivyo ni unapiga kimya endelea na maisha yako.
NimepokeaAsante mkuu, barikiwa sana🙏🙏
HakikaUsimpigie, ataona una shida nae sana. Watu wa hivyo ni unapiga kimya endelea na maisha yako.
Thank you🙏🙏.. Leo itabidi nitembelee huko nimewamisi sana kf.. Barikiwa mkuuUmenichekesha sana 😀,
Ushauri wangu ni huu👉
Biblia inasema utavuna ulicho panda, kwahvo kuna siku utatendewa wema mkubwa, kwahyo usione umepoteza.....
Kumbuka biblia haijasema utavuna ulipo panda, noo utavuna ulicho panda kwahyo usitegemee chochote kwa uliye msaidia...
Jambo la pili, jifunze kushukuru unapopata nafasi ya KUTOA kuna watu wanakosa wakuwasaidia.. kumbuka unaposaidia mtu ni kwa faida yako, wewe ndio unafaidi saana kuliko yeye kwahyo unapaswa kufurahi na kushukuru kwa kupata mtu wa kumsaidia...
Mwisho kabisa, we love yoo miss kf
Sawa sawa.Hapana, mtu mjinga ni lazima aambiwe kuhusu ujinga wake ili ajifunze na asije wafanyia wengine ujinga.
Mimi angenishukuru tu ingetosha mkuu🙏.. Anionee wivu na aliona kabisa sina hela nilimuomba mama jamani😃😃Wanawake Kama hao Ni halali kutiwa na kuzalishwa na wababa tofauti tofauti na kutelekezwa imagine umeji sucrifice malipo yamekuwa Maumivu in short huyo anakuonea wivu..
Sio kweli huyo ana hoja kwanini anampigia simu apokei wakati kajitoa sana mpaka kapoteza muda kwenda pelamio kumbe katoka . Huyo mwenye mtoto hana utuKwakua umeamua kumsaidia we msaidie Tu hayo malalamiko ni ishara ya majivuno
nipe namba yake nimpe mhuni yuko hukohuko amuongeze mtoto wa piliMimi angenishukuru tu ingetosha mkuu🙏.. Anionee wivu na aliona kabisa sina hela nilimeomba mama jamani😃😃
Asante kwa ushauri mzuri mkuu, Barikiwa sana🙏🙏Kama utaweza kukaa kimya itakuwa best zaid, kuna wakati unatakiwa uufunze moyo wako kuwa na uvumilivu( jipge kifuani na sema moyo wang kuwa na subira). Halaf endelea na mambo mengne kabisaa na sahau hayo yote na unajua ni kwann brother?? Ukimpgia simu ni kama unataka kutuliza maumivu ya moyo wako tuu kwa sababu lazma atatafuta uongo wa kukwambia. Sasa kwa kuwa uneshaona picha ( ishara) kausha kabisa na vunja urafki nae kabisa huo hana maana ya kuwa rafk and mind you akishajua udhaifu wako atakumia tuu na haswaa akiwa na shida zake tuu.
Huyo anatakiwa ajifunze kwa maumivu, next time akikosa msaada atajifunza kitu.Hapana, mtu mjinga ni lazima aambiwe kuhusu ujinga wake ili ajifunze na asije wafanyia wengine ujinga.