Sijui nifanyeje wanajukwaa


mhhh patamu hapo
 
kaka nakuambia hivi, kwanza ulikosea sana pale huyu binti alipofukuzwa kwao wewe ukamsaidia inamaana uliendelea kulea upumbavu wa watoto wa kike kwa mwavul wa mapenzi pasi kujua kwamba wewe huwez kuwa na uchungu kuliko mzazi wa binti huyu.

sitak kuamni kwamba wewe ulimuonea huruma kumbe tayari ulikuwa mfariji mtaabishaji kwa huyu binti. ungekua makin ungemsaidia arud kwao aka reconcile na wazazi wake kuliko kujibebea mzigo wa kumsomesha binti asiyejali wala kukthamini.

huyu binti toka kwao anatabia mbaya na ndio maana wazazi /walez wake walimfukuza na ulipomchukua with hizo elf 40 kwa wk ndio ulimpa wigo wa kuwa kahaba mzuri.

baada ya kukwambia hayo sasa endelea na mipango yako ya ndoa, wala asikupe presha huyu na tena mpige mkwara na ikiwezekana mchukulie rb kiwa kukutishia maisha wewe manake kwa maneno yako anaweza hata kumdhuru mkeo.

kwawanaume wengine jamani muwege mnatumia akili msijiingize kwenye mitego ya kusomesha binti with hope ya kupata returns itawakosti.
 
huna haja ya kupata presha ndoa haizuiwi kufungwa kwa ajili ya mimba .. inazuiwa na cheti cha ndoa
 
Hakuna hata mmoja; yupo jaama yangu kasomesha zaidi ya wanne lakini hadi leo ni bachela over 48 yrs sasa!

Na mimi kuna wawili nawafahamu waliishia kulia tu
 

gfsonwin aliyezama kwenye mapenzi kichwa, miguu, mikono etc hawezi kukuelewa hapo kwa red. Kwa mtizamo mwingine acha tu waendelee kuwasaidia wadada wapate elimu
 
Hakuna hata mmoja; yupo jaama yangu kasomesha zaidi ya wanne lakini hadi leo ni bachela over 48 yrs sasa!

dah huyo net yake ina matundu hadi leo 48 yz hajampata mwenzi daah pole yake
 

Kwani hilo kanisa lako husikiliza maneno ya upande mmoja tu au hata uchunguzi hawafanyi? Au kuna ukweli fulani katika madai yake?
 
Sijui ni kwa nini wanaume wanaendelea kuangukia kwenye huu mtego wa kusomesha mabinti kwa mategemeo ya kuja kuwaoa??? Hivi wapo waliofanikiwa kuwaoa mabinti waliowasomesha??

Kama wapo ni wachache sana Sangarara......wengi huwa wanaishia kulizwa!
 
Last edited by a moderator:

aisee hata mie nimemshangaa mtoa sredi khaaa! Kwa muda mfupi namna hiyo unawezaje kukutana na mtu mpaka kupanga mipango ya ndoa? Au ex ana mimba ya miaka miwili??sijaelewa!:gossip:
 
Hapo kwenye bold na mimi ndio nimepaona pana uzito kuliko thread yooote. Ni very rare kusikia mwanamke anasema ukiniacha NITAKUUA; angesema NITAJIUA ningemuelewa kwani ndivyo wanawake tulivyo. Kaka ulipenda jini si binadamu. Binti kashindikana kwao wewe ukajitia fundi wa kulea. Na usimchukulie poa huyo dada inawezekana ana matatizzo ya akili kwa statement aloitoa. Kaa chonjo.

Otherwise hawezi kukuzuia kuoa kama walivyosema wadau; ila jua una life time problem kwenye ndoa yako haswa kama hiyo mimba ni kweli yako.

Na kama walivyosema wadau huyo mchumba ulimpata lini mpaka huyu muuaji mtarajiwa akusingizie mimba? Au ulikuwa una date wasichana wawili kwa wakati mmoja? Kama ndiyo; that's bad. Kama siyo umeshindwa kujifunza tokana na makosa umekurupuka kukimbilia kuoa kabla hujamjua huyu wa sasa. She could be even worse.


 
Huyu mtoa mada kidogo ananipa shaka.. Mi ninachofikiria ni kwamba alikuwa na mahusiano na huyo Ex wake wakati teyari ana huyo mke mtarajiwa.. Sasa kitu kimekatikia anaanza kuhaha.. Jamani ukiachana na mtu achana nae moja kwa moja mwisho wa siku ndio unakumbwa na mambo kama haya.. Na huyo mtarajiwa akija kugundua kwamba mlikuwa mnakumbushana na your Ex patachimbika.. Pole yako!
 
Huyo mapepe dawa yake atekwe apelekwe msitu wa pande siku mbili kabla ya ndoa yako maana inavyoonesha anaweza akaibuka kanisan kukuaharibia ndoa yako alafu maandalizi yawe hayana maana.Huyo dada ni muhuni kwa jinsi stori inavyojieleza so nipo tayari kutoa msaada wa kamba na soletepu ili tumpeleke msitu wa Mwepande maana kwa taarifa hapa nilizonazo zinasema ule msitu bado haujafwekwa.Yaani ni chizi sana ameshazikumbuka elf 40 zako na laki 6 sita yako ndo anakuja kukutishia mimba.KAMA UKISHINDWA NIPE TENDA HII SITAKUANGUSHA ILA NA WEWE ULIWEZAJE KULILEA HILI KUNGURU LILILOSHINDIKANA NA WAZAZ WAKE?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…