Sijui niitaje huu mlo! We soma tu utaupa jina mwenyewe

Sijui niitaje huu mlo! We soma tu utaupa jina mwenyewe

snowhite

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,065
Reaction score
24,559
MAHITAJI
VIAZI VITAMU
NYAMA YA NG'OMBE/KUKU /SAMAKI(Chagua kimoja kwa mlo unaweza kubadili kwa mlo mwingine)
NJEGERE
KAROTI
VITUNGUU VIKUBWA VIWILI
TANGAWIZI kiasi
BLUE BAND vijiko viwili vikubwa
ROYCO kijiko kimoja kikubwa
pilipili manga (ukipenda)
maji ya kuchemshia nyama/kuku. kama utatumia samaki usiichemshe)

UPISHI WA NYAMA
1.kata nyama kwa vipande vidogo vidogo
2.ioshe vizuri kisha bandika jikoni usiweke chumvi
3.iache iive kisha ipua weka pembeni!

UPISHI WA NJEGERE
chemsha tu bila chumvi

UPISHI WA SUPU
1.kata karoti,vitunguu kwa vipande vya mraba saga tangawizi weka kwenye sufuria pamoja
2.bandika jikoni kabla hujawasha jiko weka kabisa blue band then vichanganye pamoja moto uwe mdogo sana!
3.chukua nyama(bila supu yake)au kama ni samaki tumbukiza samaki wabichi uliowaweka ndimu ukipenda(kukata shombo)
4.changanya kwa dk 5 hv,thn weka royco,changanya tena kwa dk2
5.weka supu ya nyama kwenye mixer yako thn funika ongeza moto iache ichemke kwa dk 5 kama ni nyama na dk 10 kama ni samaki
6.tumbukiza njegere acha vichemke pamoja kwa dk 5
ipua.

UPISHI WA VIAZI
1.menya viazi na uvioshe vizuri
2.bandika jikoni weka chumvi kidgo sana,maji yasizidi viazi funika na jani la mgomba au foil kama jani la mgomba halipatikani maeneo karibu
3.acha vichemke kama dk 20 thn jaribu kuangalia kama vimeiva kwa kubonyeza na mwiko,kama tayari ipua!
4.toa jani la mgomba na uchuje maji rudisha viazi jikoni vikiwa havina maji viache wazi ili vikauke,kisha pakua mahali ufunike vizuri ili visipoe!
ANDAA!serve it na juice yoyote
for dinner ni poa zaidi.
wakati mwingine mi huweka mihogo badala ya viazi vitamu nayo poa
au hata kutumia samaki wakavu badala ya wabichi (ila kama ni wakavu nawaloweka kwanza!)
karibu tupike na karibu kwa maswali pia!
 
Mboga chukuchuku ya maana, samaki. Nshapata lunch ya kesho, kasoro nitaweka mashed potatoes.
Very healthy, umesahau kachumbari (napenda kachumbari sikawii kunyea chai, kha!)
 
supu si supu, chuzi si chuzi..basi mie nauita mmiminiko au mchanganyiko, phew!!
 
Mboga chukuchuku ya maana, samaki. Nshapata lunch ya kesho, kasoro nitaweka mashed potatoes.
Very healthy, umesahau kachumbari (napenda kachumbari sikawii kunyea chai, kha!)
umeona enh!yani veeery veeery healthy and TASTY TOO!
AHAHAHHAHAHHA WE kichwa yako sio nzima unataka salad kwa ajili ya chai!mweh!
 
Mboga chukuchuku ya maana, samaki. Nshapata lunch ya kesho, kasoro nitaweka mashed potatoes.
Very healthy, umesahau kachumbari (napenda kachumbari sikawii kunyea chai, kha!)
mlo huu kwetu tunaita chenebatete!

cc;ameline snowhite ameline

msishangae mi kujibu leo maana post ni siku nyingi...ndo mara ya kwanza kuingia jukwaa hili!
 
Mboga chukuchuku ya maana, samaki. Nshapata lunch ya kesho, kasoro nitaweka mashed potatoes.
Very healthy, umesahau kachumbari (napenda kachumbari sikawii kunyea chai, kha!)

Hahahaaa Kunyea Chai
 
Back
Top Bottom