Konny Joseph
Senior Member
- Aug 28, 2016
- 118
- 199
Nashindwa kuelewa tusimame kwenye kauli ya yupi!!
Sielewi ni kauli ya yupi ina uhalali baina ya hawa wawili!!
Sielewi mbaya hasa kwa mujibu wa sheria hapa ni nani,baina ya wanaosemwa wanatukana viongozi mitandaoni,na huyu anaetangaza kuwapoteza hao wanaotukana viongozi mitandaoni tena kwa matamko ya wazi hivi!!
Hivi ina maana Mh.Masauni yeye hana mamlaka ya kushughulika na watu kama hawa!!
Mamlaka yake ni kushughulika na wanaokosoa serikali tu mitandaoni!!
Au kwa sababu huyu kavaa hili jokho la kinabii,ndio maana anachosema na kutenda ni sawa tu kwa mujibu wa sheria.
Serikali inapaswa ijitathimini sana.Sioni haja ya kuanza kutoa vitisho kwa wakosoaji wa serikali,ikawaacha hawa wanaovunja sheria hadharani.
Ni aibu mno!!!