Ryzen
JF-Expert Member
- Dec 6, 2012
- 7,301
- 8,706
Ama kweli dunia ina maajabu na ukistaajabubya Mussa utaona ya firauni. Watu wengine wanadai mwanadamu hata uwe na akili vipi lakini kuna muda utafanya upumbavu. Hiki ndicho ninachoweza kusema kwani wanasoka wawili wanaoshimiwa zaidi duniani wamefanya tukio ambalo huwezi amini kuwa mafundi wa mpira kama hawa wanaweza kusema hivi.
Alianza Luis Suarez, Suarez anadai kutokana na sababu za usafi ambazo pia anataka mwanae inambidi ajisaidie haja ndogo kama wanawake. Inafahamika mwanaume hujisaidia haja ndogo akiwa amesimama lakini sio kwa Suarez, Suarez huwa anakojoa akiwa amechuchumaa au kukaa kutokana na choo chake kilivyo. “Sipendi kukojoa huku nimesimama kwa kuwa mkojo unakuwa unaruka hivyo inanibidi nikae” alisema Suarez.
Pacha wa Suarez uwanjani Lioneil Messi naye alisema lake kuhusu kujisaidia haja ndogo. Messi naye ni kama anamuiga Suarez kwani naye anasema huwa anajisaidia haja ndogo akiwa amekaa. Baada ya Suarez kusema hutoa haja ndogo akiwa amekaa, Messi alionekana kushangaa akamuuliza Suarez “Haa unajisaidia haja ndogo ukiwa umekaa?mimi pia” Messi huyo alimuambia Suarez. “Nafurahi sana nikijisaidia haja ndogo huku nimekaa,usiku mzima unakuwa umelala asubuhi inapofika ukikaa na kujisaidia haja ndogo baasi ni raha tupu”.
Lioneil Messi na Luis Suarez msimu huu wameshaweka kambani magoli 44. Na wiki iliyopita walikuwepo katika kikosi kilichoshusha kipigo cha bao 6 kwa 1 dhidi ya Psg. Wanaonekana ni mapacha haswa kwani pamoja na ushirikiano wao ndani ya uwanja lakini nje ya uwanja pia wanafanana hadi jinsi ya kujisaidia haja ndogo