Sikia hii

Sikia hii

Mzawa_G

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2014
Posts
669
Reaction score
1,475
Mwezi uliopita nilialikwa harusi moja kama mgeni wa heshima, tena mwaliko ulikuwa wa simu tu sikuletewa kadi, mambo ya minuso na madikodiko huwa sifanyi makosa kabisa, harusi ilikuwa kwenye moja ya ukumbi maarufu tu kwa hapa Dodoma.

Nilipofika getini wahudumu wakanipokea na kulikuwa na mabaunsa kadhaa. Wakauliza kadi, nikawambia mie ni mgeni wa heshima.

Wahudumu wakanielekeza kwakunionyesha niingie mlango mmoja uliokuwa mbele wakasema nitaona maandishi, Nilipoingia nikaona pameandikwa kulia ni ndugu wa maharusi, kushoto ni wageni waalikwa, nikaenda kushoto maana mimi nimwalikwa.

Nikakuta mbele kuna mlango mwingine umeandikwa kulia wenye zawadi kushoto wasionazawadi, mimi sikuwa na zawadi zaidi ya suti yangu tu ya kibobezi, nikakata kushoto.

Nikakuta tena mlango umeandikwa kulia wanawake kushoto waume, Mie na suti yangu nikakata kushoto, ghafla nikajikuta nimetokea nje mtaani...na kwanyuma nikasikia mlango ukifungwa paaah!

Sikuhoji mtu yeyote, nikaanza safari kurudi nyumbani....

Huwa najiuliza sana, kama harusi tu tunafanyiana hivi, je mengine itakuwaje?, Siku hiyo hakika nililala na njaa hivihivi, asubuhi kumekucha nikajicheka mwenyewe.
 
😹😹😹😹😹😹😹😹😹😹😹😹😹hahahahahhhhh nimecheka kinafki ile noma

Back
Top Bottom