Sikia Kauli za ' Kuudhi ' za Watanzania wasio na haraka pale ukiwa unawapita barabarani huku Wao wakiwa wala hawana haraka!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
1. Unajifanya una haraka sana kwanini basi hukulala tu huko huko tokea jana?
2. Kama una haraka sana na unataka Kuwahi Kodisha basi Bombadia au Drimulaina Mpuuzi Wewe!
3. Waliowahi sasa wako Makaburini Wewe unachoharakisha hadi unatugonga ni nini?
4. Huna lolote Spidi yote hiyo unawahi Kumkopa Mtu huko!
5. Siku zingine ukitaka kuwahi uwe unameza Injini ya Jet ili utupite humu kama Mshale sawa?
6. Naona unataka Kushindana kuwahi kama Inzi wa Chooni!
7. Kwa Miguu yako hiyo iliyoelekea Kushoto unategemea utawahi kweli huko unakoenda?


Maneno mengine kama yapo mtayaweka nyie ila Mimi kwa wiki hii nimeyasikia haya tafadhali.

Nawasilisha.
 
Noma mkuu watz ni noma
 
Noma mkuu watz ni noma

Mkuu tokea Wiki hii ianze nimekita Kambi maeneo ya Ubungo ebwana mbavu zangu zinapata sana taabu kwa Kuteswa na Kucheka hasa kwa Kauli hizo za Watanzania. Asikudanganye Mtu kama kuna Watu / Raia ambao ' wamebarikiwa ' kupiga ' Madongo ' tena ya Kuudhi na Kutukuka ambako kama ukiwa na hasira za karibu kama GENTAMYCINE kila siku unarusha ngumi basi ni Watanzania. Na kibaya zaidi hao ambao huwa wanayatoa hayo ' maneno shombo / maneno madongo ' huwa wala hawaangalii wanayemuambia ana rika gani yaani Wao yoyote atakayewapita tu mbele yao ' atayakoga ' hadi atajuta kwanini aliwapita kwa Kasi barabarani.
 
Kama barabara ni moja basi wanyuma akizidisha honi, wambele utamsikia


'Pita juu'.. Anatoa na mkono kwa dirishani kumuonyeshea ishara ya kupaa kwa juu.


Wengine utasikia.. "una haraka kama unaoga nje"
Huwa nafanya hivyo kila mara yawezekana uliniona mim halafu natoa na kidole kimoja cha kati.
 
Huwa nafanya hivyo kila mara yawezekana uliniona mim halafu natoa na kidole kimoja cha kati.
Alafu hii tabia tunayo wengi wetu unakuta magari sio yetu tumeazima tu.

[emoji125] [emoji125]
 
Alafu hii tabia tunayo wengi wetu unakuta magari sio yetu tumeazima tu.

[emoji125] [emoji125]
Hahaha kwangu mie ni miaka ya 2000. Nilishaacha kuendesha baada ya kuishi nchi ambazo kuendesha ni hatarishi ila nikipeleka watoto IST Upanga zamani walikuwa wanasema mama unaendesha kwa kasi. Those were my days. Sasa hata kushika usukani siwezi.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] hii tabia ninayo sana ya kuwatusi watu wenye haraka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…