MR LINKO
JF-Expert Member
- Aug 20, 2016
- 3,034
- 3,526
Habari wakuu natumaini wote ni wazima.
Iko hivi nilitoka nikaenda village ndani ndani kabisa kiasi kwamba hata huduma za kawaida kuzipata ni mpaka upande boda boda maana hata usafiri wa gari hamna na unakuta nauli ni kama 7000 hivi kama wakikuonea huruma basi ni 5000 kama unaenda na kurudi.
Basi nikapanga safiri nikaanza nika panda basi nikawapa taarifa Mungu mwema nikafika salama, walinipokea kwa upendo kama unavyojua kijijini lazima wakualike na kukuchinjia kuku na ugali wao mkubwa kama wa mtu 4 hivi.
Picha linaanza kuomba maji ya kuoga aisee ilikuwa ni hatari nikaletewa maji nusu ndoo na maji ya rangi ya maziwa nikaona ngoja nioge sio kesi. Nikaulizia sehemu ya kulala wakanipeleka nyumba ya udogo imejengwa na fito na kubandwikwa matope na ni fupi nikisimama nakaribia bati na mlango unafungwa na mti nikaona mi mwenyewe kontawa nikaangusha kiroho safi tu.
Kesho asubuhi nikaitiwa uji nikaletewa jagi zima na kikombe nimeanza kunywa hamna sukari ikabidi niwaambie kuwa wachukue pesa wakanunue hata kilo 3 ila wakadai duka liko mbali sana. Nikaona sio kesi ikabidi nitulie nikaugonga kikombe kimoja maisha yakasonga.
Mchana kama kawaida samaki wa kuchemsha tu hamna nyanya wala mafuta na ugali mlima balaaa nikagusa kidogo kisha nikasema nimeshiba walicho niambia ni kuwa nitazoea wananipa muda nitakuwa kama wao, tukacheka tukafurahi maisha yakasonga.
Kwa pale ratiba ziliendelea kama kawaida kumbe ninavyo zidi kula na utumbo unapanuka na naendelea kuongeza ratio ya kula ikafika nikawa nakulaa sana yani tunaenda sawa na wazawa, kwa kipindi hicho niligoma kunywa maji yao maana nilikuwa siwaelewi wanachota sehemu ngombe wanapo kunywa kisha wanaacha yanapoa ndo wanakunywa.
tokea nimekaa ni kama week ila sikuwahi pata haja hata kidogo sasa ile week ya pili kuanza kwakuwa nilikuwa mgumu kunywa maji hapo ndo nilijua umuhimu wa maji kwa kila kitu. nikamuomba mwenyeji wangu anipe maji ya kwenda toi akanipa kwenye ka kidumu nikaulizia chooo akanionyesha pori ambalo ndo toi nikaenda huko.
Aiseee usiombe yani kwa mateso yale nilijuta kwanza "NAWAPONGEZA WANAWAKE WOTE WANAO ZAA KWA UCHUNGU" ile kitu nilifika kila nikijaribu ngoma ngumu ikafika nasimama nusu kuchuchuma siwezi kusimama siwezi mpaka machozi yakaanza kunilenga huku nikitafakari jinsi ya kufanya (kidogo nirudi kwa mwenji nikiwa niko nimechuchumaa nikatamani hadi kupiga ukunga) nilikaaa porini kama lisaa na nusu viungo vyote vina umaa maana nilikuwa kwenye msoto mkubwa sana. Mwenyeji alijua nimeenda kutembea kumbe nilikuwa leba ndogo.
na porini ukiangalia kuna mtu kashusha mkono wa mtoto aisee lile sio gogo ni zaidi ya gogo nikasema nikikata kama hili nakufa hapa hapa.
Ushauri maji ni kila kitu hata uende wapi hakikisha unakunywa maji yani kwa tukio lile nilituma boda anilete katoni ya maji maana sio kwa balaa lile lililo nikuta mpaka leo lazima niwe na maji pembeni piga uwa.