Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
wangazija ni wabantu,kwa hiyo lugha wanayozungumza itakuwa inafanana sana na hizi lugha zetu ambazo ndizo ziliunda lugha ya kiswahili pamoja zilichanganya na lugha ya kiarabu,kweli kile ni kiswahili niliwahi kutembelea Commoro zamani walishangaa sana kuona kuwa nilikuwa ninawasikia wakiongea lugha yao kwa asilimia kubwa sana.Wale ni ndugu zetu wenzetu.M/Mpamba.
Hapana mkuu, Kingazija ni lahaja ya Kiswahili. Inajumuishwa katika kundi la lahaja za Kusini na Pwani...
Hi haya yote ya kujiita lahaja ya watu wa pwani yote haya yanajitokeza ktk kutaka kuukacha ubantu tuu na sio vinginevyo,nimeona sana jamaa wa pembezoni ya pwani hususani east afrika wanapenda sana kujitafutia nasaba nyenginezo ambazo hata asili nazo hawana na hawazijui ili waonekane wao hawana ubantu ndani ya nenes zao najua hii statement yangu itawakwaza baadhi ya wachangiaji humu ndani lakini ukweli ndio huo.M/Mpamba.
Sasa kiswahili sio lugha inayotokana na kibantu?hii mambo ya sijui lakhaja sijawahi sikia hata siku moja,watu wa pwani ya coast ya east Africa walioanza kuishi hizo pande wote walikuwa ni watu wa kabila za wabantu na sio vinginevyo kwa hiyo lugha yoyote itakayo jitokeza itakuwa asili na chimbuko lake ni kibantu.End of story.
Nimetumia neno nasaba yaani wanapenda sana kujipa unasaba mwingine na yote ni kutaka waonekane ni watu tofauti na wengine hapa Afrika ya mashariki,kwa mfano baadhi ya watu wanapenda kujinasibisha na watu wa mataifa mengine na mfano mkubwa ni hapa hapa kwetu kuna baadhi ya wenzetu eti na wao wanajiita kuwa wao ni wahindi au waarabu sijui yote haya yanatokea wapi au ni kasumba gani tunazo sisi wabongo(najua hii comment itaweza leta controversy moja kali saana kwani nimegusa ktk mioyo ya watu wa namna hiyo )nimewahi kusikia kijiweni pale mjini Mombasani nchini Kenya jamaa wanawaita watu wengine eti waafika,mijiafrika,hata huko huko Comoro nako kasumba hiyo imekithiri,mfano ukitokea Tz wanakuuliza vipi huko Afrika hawajambo?yaani wao bara au nchi yao haikuungana na bara la Afrika,kwa hiyo sio waafrika hata sijui wako maeneo gani.Kasumba ka hizo ni nyingi sana hata pa kuanzia hakuna.M/Mpamba.