Sikiliza hiki kisa huenda ukatoka kitu cha kukusaidia katika maisha yako

Sikiliza hiki kisa huenda ukatoka kitu cha kukusaidia katika maisha yako

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
557
Reaction score
858
Kuna dogo mmoja tulifahamiana nae humuhumu ndani, alikua very charming na mtu wa watu sana, dogo alikua anauza account za biashara za instagram, yaani yupo yeye na wenzake wanakuza account from the scratch hadi inakua kubwa.

Wengi tunajua sometimes account ili ikue inabidi ulipie hadi hela, sasa madogo wao walikua wana account za mambo ya wanyama, utalii na nyingine za vichekesho tu, wanazikuza zinafika mpaka 80k huko alafu wanaziuza.
20250222_092549.jpg


Siku moja jamaa yangu alikua akitafuta sana account ya instagram yenye followers wengi, basi mimi kwakua namfahamu dogo nikamcheki na kipindi hicho huyu dogo alikua anasoma shule ya secondary.

Dogo akanipa ratiba yake kwakua yupo shule, dogo alikuja siku baada ya kutoka shule na tukaja kupiga stori na kufanya biashara ya ile account, wakati tuko pale nikawa namuuliza dogo anawezaje kukuza akaunti hivi, basi chakushangaza dogo akanionyesha akaunti yake ya WhatsApp, akipost tu just now ana views 300, siku nzima dogo anapiga 3400 sometimes mpaka 4000.

Kiutani tu nikamwambia dogo unachezea utajiri😅, basi ile siku tukamaliza na tukaishia zetu, yule dogo alikuja kumaliza shule na akanitafuta akisema “blaza nasubiri matokeo ya form 6 lakini hali ngumu na sina cha kufanya, nikisema nisubiri mpaka matokeo ya chuo kikuu nitakua vibaya zaidi, nataka nifanye biashara ila sijui naanzia wapi!

Nikamwambia tafuta idea tatu za biashara ambazo wewe unazipenda na ambazo unahisi wewe utazimudu, nikamwambia ukiwa tayari njoo dukani Mwenge tutayajenga, basi mimi nikawa tayari nilisha sahau ila niliona dogo yupo serious sana, siku moja akanipigia simu akaniambia blaza next week siku fulani nakuja tuongee sasa nipo tayari.

Ile siku ilipofika dogo alikuja mpaka dukani, akaniambia direct blaza mimi nataka nifanye biashara ya kuuza Simu, sasa nielekeze naanzaje….😅

Hii nikiipeleka instagram sipigi hela?🤣

Nazingua bana, nikamwambia dogo chakwanza una utajiri wa kwanza ambao ni views wengi WhatsApp, mbili una nia, na tatu unauwezo wa kukuza account za instagram ambazo ndio platform kubwa ya bishara nyingi na ina soko kubwa la biashara anayotaka kufanya.

Dogo akasema mimi ntakaa ofisini kwako ili nijifunze hapa, lakini nilimkatalia sababu niliamini hiyo sehemu namtafutia atashine kwa muda mfupi kwa kipindi kile, na palepale nilichukua simu yangu na kumpigia jamaa yangu alieko sinza na kumwambia kwamba nakupa kichwa machachari sana, jamaa yangu akaniambia mimi mawinga wamejaa na si muda mrefu nataka kuwapunguza wengine. Nilikata simu ila sikumwambia dogo tajiri kaniambia nini ila nilimwambia aende pale aonane na mtu fulani alafu awe karibu naye.

Dogo alikua msikivu na alifika pale akawa anafanya vizuri sana, siku moja nilipokwenda kuwasalimia tajiri ake akaniambia kijana yuko vizuri na ndio anaongoza kuuza simu pale dukani kwake, nikakaa nae nikampa madini mengine tena, maana dogo matokeo ya chuo yalitoka akawa hajui aende chuo au abaki kukimbiza biashara, sikukumbuka nilimshauri nini ila maeneo madogo alipokea ushauri katika mji mkuu mwaka ujao, mdogo mdogo alipokea ushauri katika jiji lake. ananifata na ananisalimia kwa sana na alikua kila akiniona haachi kunishukuru hadi siku moja nilipo mwambia acha kunishukuru sababu mimi nilifanyika daraja tu.

Dogo akanipa mipango yake kwamba kwakipindi kile alikua anahela ya kununulia crown, dogo alihama kwa wazazi wake akahamia sinza, hela alikua anapata na alikua ni dogo mwenye heshima na alijuana na watu wengi kwa muda mfupi sababu pia alikua na bidii sana.

Mungu amrehemu dogo maana kwa sasa hatunae, Mungu alimpenda zaidi.

Nimeshare hii stori na vijana huenda kuna jambo wakajifunza kupitia dogo.

Nimeitoa kwa Boniface Chengula
Mtandao wa X (twitter)
 
Madogo wakianzaga hustle wakimaliza six huwa wanakua vizuri, wengi wanakuaga na mchecheto wa chuo. Wakienda chuo sijui huwa wanaliahwa nini wakija mtaani wanakua sio wale tena.
 
Back
Top Bottom