Sikinde ya Kweli!!!!!

Kitu leyland cd.
Sio bendi za siku hizi hawana hata mabasi, wanaishia kukodi ma kosta ya mwenge kariakoo
 
Mnazi mmoja hapo na hiyo nyuma ni STARLIGHT CINEMA wakati huo siku hizi STARLIGHT HOTEL
 
jamani jamani jamani.. this is beautiful THREAD.. natamani kila picha ikawa na maelezo angalau kidogo!!
it was real real gud..
 
hapo bendi ni sikinde wana DDC MLIMANI PARK ORCHESTRA. sifa zao zitanifanya nijaze page yote hapa ila ningemuwa pedeshee ningenunua vyombo vya m100 halafu wale wakongwe wote wa nginde waliopo ningewakabidhi hivyo vyombo akiwemo WAZIR ALLY (kissinger) kwenye keyboard wajifue miezi mitatu halafu ningeandaa tamasha kubwa sana pale uwanja wa taifa ningealika bendi mashuhuri nyingi sana tu mpya na kongwe wakongo kwa wasauzi wa nigeria wamarekani. ningealika family za wanamuziki wote waliopitia nginde mpaka leo, mpaka wawakilishi wa family za waliotangulia mbele za haki halafu tamasha likapigaa hapoooo usiku kucha. lengo ni mapato ya kiingilio yawe testimonial kwa wana sikinde woote wagawane mshiko atleast kila mwana muziki awe na 5m bank jamani wamefanya kazi kubwa sana tu kwa hii nchi lkn maisha yao hayaridhishi kabisaaaa.
 
tufurahi tufurahi na wanasikinde tucheze leo ngoma ya ukae, ukitaka tufurahi kila jmosi njoo uburudike na wana sikinde oyee, Abel mulenga...........bitchukaaaaaaaa, gurumoooooooooo mungu awape siku zaidi za kuishiiii
 
aah mi naona watu tu minywele mingi nguo zime wabana swaga hakuna kabsa halafu watu wana wasifiiiia...
 
Hata huyu hamumjui?



Huyu hapa kulia kabisa....majuzi tu na wanawe

 
Hapo ni full kaswende , Kisonono na gono, hakuna Ukimwi! madada walikua wana chakachuliwa bila woga.
 


Mzee Joseph Nyerere alikuwa mpenzi sana wa Vijana Jazz Band. Nakumbuka siku za Jumapili ambapo Bendi ilikuwa na onyesho lake lililoitwa Vijana Day mara nyingi ungemkuta pembeni akisikiliza muziki na pengine akiomba special request. Ilikuwa ni burudani pale ambapo aliamua siku hiyo kucheza maana alikuwa na staili ya peke yake iliyofanya mtu apende kumuangalia. Historia inasema alisoma Tabora Boys na alikuwa Band Master wa bendi ya shule na alipendwa sana kutokana na mbwembwe zake alipokuwa akiongoza na kifimbo cha Band Leader. Mzee Joseph aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa TANU Youth League. Pichani akiwa jukwaani na Marehemu Hemedi Maneti katika Ukumbi wa Vijana Kinondoni, kwa mbali nyuma anaonekana Aggrey Ndumbalo akiwa ameshika gitaa na Said Hamisi muimbaji wa Vijana akiwa napiga makofi, wote wamekwisha tangulia mbele ya haki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…