Hii ni special kwa wazee wenzangu tu.
kama wewe hukuwepo wakati huo soma upate idea tulikuwa tunafaidi nini!
Tulipokuwa primary,unakumbuka?
Tujikumbushe kwa Upande wa vitabu vya Kiswahili, as huko nako ilikuwa burudani tupu. stori kama KIBANGA AMPIGA MKOLONI, SIZITAKI MBICHI HIZI,SIKU YA GURIO KATERERO,BENDERA YA TANZANIA,ANDUNJE( mtoto mdadisi), NGANENEPA ANGATWA NA NYOKA,AHADI KUMI ZA MWANA TANU na nyingine nyingi zote ilikuwa burudani tupu.
Kweli wakati ule mtaala ulikuwa umetulia, kwa sasa hivi sifahamu mitaala ikoje lakini nakiri mtaala katika somo la kiswahili, ulikuwa umetulia.
Nimalizie kwa beti ninazozikumbuka( japo sizikumbuki vizuri sana) kutoka katika shairi la sizitaki mbichi hizi
Hadithi inayokuja, ni ya sungura sikia
hadithi uliyongoja leo ninakuletea
Alitoka siku moja njaa aliposikia
njaa aliposikia sungura nakuambia
Siku hiyo akaenda porini kutembelea
akayaona matunda mtini yameenea
sungura akayapenda mtini akasogea
Mtini akasogea sungura nakuambia
SIZITAKI MBICHI HIZI, sungura akagumia
naona nafanya kazi bila faida kujua
yakamtoka machozi matunda akalilia
Matunda akalilia Sungura nakuambia
Usifanye utani mkuu, kile Kiswahili tulichosoma sie enzi hizo kilikuwa kimetulia sana! Siyo sasa, wanetu hawajui tofauti ya ndiyo na ndio au Hapa na apa ama Hicho na hiko. Yaani hapa umenikuna kinoma.
Kwanza madarasa yale ya mwanzo kulikuwa na vitabu murua sana, kama kile cha Paulo na Selina (darasa la pili), Kuna hadithi za Kinango na Nzige, Heri Mimi sijasema na kadhalika. Ukija darasa la tatu ndio unakutana na akina Andunje, Nondo Mla watu, Twende Tukawinde,
Jogoo Aliyesema (hadithi ya Pazi) na Sadiki na Sikiri.
SHAIRI LA SADIKI NA SIKIRI
Sikiri mimi masikini
Uvivu wangu nyumbani
Ukiwa huu wa njiani
Nakufa hapa kwanini?
Sadiki sasa ashiba
Chakula kingi kwa baba
Nirudi tena kwa baba
Nakufa hapa kwanini?
Pia kitabu hiki kilikuwa na shairi la kuukaribisha mwenge, kama kuna mtu analikumbuka basi si vibaya akatukumbusha
Ukija Darasa la Nne ndio unakutana na Kibanga Ampiga Mkoloni, Ndoto ya Kimweri (chifu wa Wasambaa), Mkwawa Shujaa, Barua Kwa Mjomba Mndolwa na Siku ya Gulio Katerero (hadithi ya Kiiza). Shairi la kitabu hiki linaanza hivi:
KAMA MNATAKA MALI
Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali
Wakataka na kauli iwafae maishani
Akatamka mgonjwa, ninaumwa kweli kweli
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali
Roho naona yachinjwa, Kifo kimenikabili
Kama mnataka mali, mtayapata shambani
Darasa la tano napo kulikuwa na mahanjamu yake. Nakumbuka hadithi kama ile ya Safari Yenye Mkosi, Vijana Wapiga Kambi Ngulwi, Ukakamavu, Kapulya Mdadisi, nakadhalika.
SHAIRI LA KITABI HIKI LINAANZA HIVI
Tumeizika elimu, elimu ya kizamani
Elimu ile haramu, maana ya kikoloni
Imetuishia hamu, kuiga ya ugenini
Elimu yetu ya sasa yawafaa wananchi
Kitabu cha Kiswahili cha darasa la sita sikikumbuki vizuri, tulikuwa na mwalimu bomu sana ila nitajitahidi kukumbuka, nadhani kulikuwa na mada moja inahusu walowezi.
Kwa upande wa darasa la saba mambo yalikuwa poa sana. Kulikuwa na mada kama, Chuo Kikuu, Brown Ashika Tama, Jiji la Dar Es Salaam nk. Kulikuwa na mashairi mawili katika kitabu hiki, moja linaanza hivi:
Ninaye ndege mzuri, mrembo wa Kupendeza
Rangi zake mashuhuri, ni nne nawaeleza
Ndizo rangi za fahari, urembo kuutimiza
Ndege huyu ndege gani, hapa Kwetu Tanzania?