Siku 100 za Rais Samia kwa kasi na viwango

Mohamed Ismail

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
224
Reaction score
236
Kimya kina mshindo, Watu wanasema Mlimwengu huoni? Mbona husemi? Mlimwengu nilichagua kutumia milango yangu ya fahamu vizuri kutathmini yanayofanyika.

Baada ya dhiki ni faraja. Tulipata msiba wote, tukahuzunika wote na ikawa hakuna wa kumfuta machozi mwenzake.Baba yetu Hayati Magufuli alipotuacha ilibaki kitendawili kwamba viatu vyake nani atakayevivaa, hiyo ndio ilikuwa kiu ya watanzania wote wanaoipenda nchi yao.

Awali ya yote nimshukuru huyu Mungu wetu ambaye aliumba mbingu na ardhi pamoja na wanadamu. Huyo Mungu ambaye ndio msanii mkuu, aliifinyanga Tanzania na akaibariki kwa rasilimali nyingi. Akatupatia mito,maziwa, bahari, milima yenye kuvutia, mbuga za wanyama, Madini mbalimbali na mandhari ya kuvutia. Tusiposhukuru wakati mwingine tunamkosea. Huyu huyu Mungu wetu hakuishia hapo akatupatia viongozi wa kweli. Akatuletea Nyerere akaona haitoshi akatupatia Mwinyi bado akazidi kutupendelea akatupa Mkapa. Taifa hilohilo akaliongezea tabasamu akatupatia Kikwete, tukiwa bado tunaendelea kuishi akatutabaruku Magufuli. Huyo huyo Mungu akatupatia Suluhu watanzania ambaye ndio baba yake Samia.

Mama yetu Samia baada ya siku 100 za uongozi wake imesababisha watanzania tujue tuna Rais wa namna gani. Mimi siku zote ninaimani na mama. Mama amekuja kipindi muafaka kabisa kwa ajili ya kuja kuponesha vidonda ndugu. Leo hii watanzania wana furaha tu sura zao zimejaa tabasamu. Vyama vya kisiasa siyo uadui, uzalendo siyo kuwaumiza wenzako. Kila mtu anachapa kazi kwa amani. Wafanyabiashara wanaona fahari kuwa katika nchi yao hata watumishi wa umma nao wana tabasamu ndani kwa ndani.

Katuletea Bajeti kuu ya taifa ya 2021/2022 ambayo itawafanya watanzania wote washiriki kuijenga nchi yao na hii itaongeza wivu mkubwa wa taifa lao. Tanzania lazima ijengwe na watanzania wenyewe. Hata majirani zetu na ndugu na jamaa wa mataifa mengine wanathibitisha hilo na wako tayari kufanya naye kazi. Hii ndio diplomasia ya kiuchumi.

Taifa limempata mama mchumi ambaye anaijenga nchi kwa kuongeza miradi na kuiendeleza ile ambayo ilikuwa ilishaanza. Nikianza kuitaja na faida zake muda hautoshi ila tutakua tunazidi kukumbushana. Mama wewe endelea kufanya kazi mambo ya kufanya maombi tuachie sisi.

Nidhamu ya uongozi makazini, unatupa somo la uongozi kwa sasa viongozi wanaheshimiana mdogo anamuheshimu mkubwa na mkubwa anamuheshimu mdogo. Nikikaa kimya wanasema mbona nimekaa kimya sasa nimeamua kusema.

Mama wewe ni mtu na nusu umesema wazi unaomba kukosolewa ukaitaka Mahakama ifanye kazi yake baadae ukaligeukia Bunge na kuwatia hamasa waendelee kuikosoa serikali na kuijenga pia. Umekubali kupokea pongezi na spana kwa pamoja.* What a leader*?

Mlimwengu nilitaka niseme kidogo tu kuhusu mama ila nadhani hapa kazi ndio imeanza. Sitaacha kuelezea mazuri yako unayoyafanya. Naomba kwa hilo unisamehe maana sina Rais mwingine zaidi yako na sina Tanzania nyingine zaidi ya hii unayoiongoza. Rais ni mmoja ambaye ni Samia na Tanzania ni moja ambayo ni Tanzania.

Nitoe Rai kwa watanzania wote tuchape kazi na wote tushiriki katika kuijenga nchi yetu. Hakuna mwenye hatimiliki na taifa hili hivyo hili ni suala la watu wote kushiriki.
#Siku100zamoto
#Tanzaniayangu
#mlimwengumimi

Imeandikwa na
Mohamed Ismail Rwabukoba
 
Well said Mkuu, Mother akiendelea hivi atatuacha pazuri sana. Hatumii nguvu wala vitisho lakini unaona kabisa viongozi wa chini yake wanamuheshimu (siyo kumuogopa).
 
[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Back
Top Bottom