Dive
JF-Expert Member
- Mar 7, 2013
- 895
- 1,489
TAMTHILIYA ya askari polisi wa kike Kenya, Caroline Kangogo, imefika mwisho, lakini haijaeleweka. Ni sawa na filamu yenye msisimko mwanzoni, ikakosa mwisho wenye kueleweka. Caroline alikuwa na daraja la Koplo (Corporal), kwenyeJeshi la Polisi Kenya.
Caroline ni jina la ubatizo. Nyumbani kwao alipozaliwa, aliitwa Jemtai. Hivyo, kwa ukamilifu, jina lake ni Caroline Jemtai Kangogo. Tamthiliya yake yenye utata mkubwa Kenya, ilidumu kwa siku 11, kuanzia Julai 5 mpaka 16, mwaka huu. Kisha, akakutwa amefariki dunia, bafuni, nyumbani kwao.
Julai 5, mwaka huu, saa 2:40 asubuhi (Afrika Mashariki), ilikuwa Jumatatu, ofisa wa polisi, Sajenti Joseph Ologe, mkazi wa nyumba za polisi za Kasarani, aliripoti Kituo cha Polisi Nakuru, kwamba alipokuwa njiani kwenda kazini, aliona gari Toyota Corolla, lenye namba za usajili KBV 735U, likiwa limepaki pembeni ya barabara. Gari hilo lilikuwa na vioo vilivyoharibika, injini ilikuwa bado inawaka. Yaani gari halikuwa limezimwa mpaka wakati huo.
Sajenti Ologe, alieleza kuwa aliweza kulitambua gari hilo kuwa ni mali ya askari polisi mwenzake, Konstebo John Ogweno. Ologe akabainisha kwamba alipochungulia ndani ya gari kupitia dirisha lililovunjika, alimuona Konstebo Ogweno, akiwa maiti tayari. Alipigwa risasi na kufariki dunia. Muda huo alipobaini Ogweno kauawa ilikuwa saa 1 asubuhi.
Ripoti ya uchunguzi kwenye eneo la tukio, ilikuwa na majibu haya; Konstebo Ogweno aliuawa kwa kupigwa risari ya milimeta tisa, pembeni ya gari, kulikutwa na jiwe pamoja na chuma, ambavyo vilibeba tafsiri kuwa ndivyo vilitumika kubomoa vioo vya gari lake. Konstebo hakuwa na bastola yake, ingawa mfuko wa kuhifadhia (holster) alikuwa nao. Hiyo ilijenga picha kwamba aliyemuua ndiye aliondoka na bastola yake.
Uchunguzi wa awali ukabaini kuwa bastola iliyotumika kumuua Konstebo Ogweno ni Ceska yenye namba 94676. Uchunguzi huo ambao ulifanywa na maofisa wa kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai, Kaunti ya Mashariki, Nakuru, ulikuta simu ya mkononi. Walipoichunguza, walibaini mmiliki wake ni Koplo Caroline. Na polisi walikuwa wakifahamu kwamba Koplo Caroline na Konstebo Ogweno, walikuwa na uhusiano wa kimapenzi.
Wapelelezi walipokwenda nyumbani kwa Caroline, hawakumkuta. Walipopekua ndani, hawakukuta silaha yoyote, ila baadhi ya nguo za Ogweno zilikuwepo chumbani kwa Caroline. Hiyo ikaleta tafsiri kuwa Konstebo Ogweno alikuwa na kawaida ya kulala nyumbani kwa Caroline. Nyumbani kwa Ogweno hawakukuta silaha wala nguo ya Caroline.
Kutokana na mazingira tata, Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kenya na Idara ya Usalama wa Taifa Kenya, waliingia kazini kufanya uchunguzi wa kifo cha Ogweno. Swali kubwa likawa; mbona Caroline hajulikani alipo? Zingatia, simu ya Caroline ilikutwa eneo la tukio.
Julai 6, mwaka huu, ilikuwa Jumanne, Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kenya, ilitoa taarifa kuwa Koplo Caroline ndiye alikuwa mshukiwa mkuu, hivyo ilitakiwa apatikane kwanza yeye, ili kuelekea kupata ukweli wa kifo cha Konstebo Ogweno.
Baada ya DCI Kenya kutoa taarifa hiyo. Siku hiyohiyo (Julai 6), mmiliki wa Hoteli ya Dedamax Kimbo, Peter Kiumi Mugeshi, alipiga simu Kituo cha Polisi Mugera, nje ya Jiji la Nakuru, ndani ya Kaunti ya Nakuru. Mugeshi aliripoti polisi kuwa kuna mtu alikutwa chumbani, hotelini kwake, akiwa amekufa.
Mtu huyo aliyekutwa amekufa chumbani, hotelini Dedamax, ni mwanaume, mfanyabiashara. Jina lake ni Peter Njiru Ndwiga, umri ni miaka 32. Taarifa zikaonesha kuwa Ndwiga, alichukua chumba namba 107, saa 10:22 alasiri, Jumatatu (Julai 5). Alipokaguliwa, mfukoni alikutwa na risiti ya Shilingi za Kenya 3,020, sawa na Sh65,000 za Tanzania.
Risiti hiyo ilitolewa na Hoteli ya Jogoo Kimakia Country, iliyopo Thika, Kaunti ya Kiambu. Uchunguzi zaidi ulibaini kuwa risiti hiyo mfukoni mwa Ndwiga, ilitolewa kwa malipo ya kibenki. Kadi ya benki iliyotumika kulipa ni ya Koplo Caroline. Risiti ni ya Julai 5, saa 9:29 alasiri. Wafanyakazi wa hoteli hiyo wilitoa ushuhuda kwamba Caroline alikula chakula cha mchana, hotelini hapo.
Kwa matukio hayo, DCI walitoa taarifa kuwa Koplo Caroline, ni mtu hatari aliyekuwa na silaha tayari kwa kuua. Walionya watu, hususan wanaume kukaa chonjo. Taarifa ya DCI ilibainisha kuwa Koplo Caroline aliwahadaa wanaume na kuingia nao hotelini, kisha aliwaua. Ikatolewa namba ya kupiga simu bure, 0800722203, kwa yeyote aliyekuwa na taarifa za Caroline.
Uchunguzi wa miili ya marehemu, Konstebo Ogweno na Ndwiga, ulibainisha kuwa sababu ya vifo vyao ni kuvuja damu nyingi, baada ya kupigwa risasi moja kila mmoja kichwani. Ilibainishwa kwamba risasi hizo zilipigwa kwa ukaribu.
Julai 16, mwaka huu, ilikuwa Ijumaa, asubuhi, mwili wa Koplo Caroline, ulikutwa bafuni, nyumbani kwao, Iten, kaunti ya Elgeyo Marakwet, ukiwa na jeraha la risasi. Kisha, ukapelekwa Hospitali ya Iten na kuhifadhiwa kwenye chumba cha maiti, mochari.
Msemaji wa familia ya Caroline, Robert Kipkorir, alieleza kuwa walimkuta mtoto wao akiwa amekaa, amenyoosha miguu, mwili wake ukiwa na jeraha la risasi, ingawa hawakusikia mlio wakati inafyatuliwa.
Kipkorir alisema, walitamani Caroline angejitokeza ili ukweli ujulikane, lakini walisikitishwa mno walipomuona akiwa maiti. Kipkorir aliongeza kwamba Caroline alikuwa mtu mzuri, mwenye hofu ya Mungu, na hakuwahi kuwa na rekodi mbaya, hivyo, walishangazwa kuhusishwa kwake na mauaji. Mwisho, Kipkorir alitoa pole na kuomba radhi kwa familia ambazo ndugu zao waliuawa.
Utata; Caroline amekufa. Wengi wanaamini alijiua. Je, kama aliuawa na kupelekwa kuhifadhiwa kwenye bafu la nyumba ya familia yao? Inaaminika ndiye aliwaua Ogweno na Ndwiga, vipi kama muuaji ni mwingine, ila yeye aliingizwa kimazingira?
Sababu ya mauaji ni nini? Caroline ni askari polisi, anajua kila kitu kuhusu ushahidi. Ni kwa nini aliacha alama zake kwenye kila tukio la mauaji? Simu yake ilikutwa nje ya gari la Konstebo Ogweno, kisha risiti iliyolipiwa kwa kadi yake ya benki, kwenye mfuko wa Ndwiga.
Je, mara zote hizo mbili ni bahati mbaya au alitaka ajulikane kuwa ameua? Kama ndivyo, mbona hakutoa sababu ya kuua? Vipi, ikiwa wauaji ni wengine kisha wakaacha alama za Caroline ili yeye ndiye aonekane mtuhumiwa?
Kama wauaji ni wengine na sio Caroline; je, shabaha ya wauaji ilikuwa kumuingiza matatani Caroline au walikuwa na visa dhidi ya waliouawa ila wakamtengenezea mazingira Caroline ili wao wabaki salama? Mpaka sasa jamii inaamini Caroline ndiye muuaji, sababu ya mauaji haijulikani. Ni tamthiliya ya giza, yenye utata mwingi.
CAROLINE NI NANI?
Kumbukumbu za Jeshi la Polisi Kenya, zinaonesha kuwa Caroline, ambaye mpaka anafikwa na mauti alikuwa na umri wa miaka 34, aliajiriwa rasmi na jeshi hilo Januari 20, 2008. Januari 20, mwaka huu, alipandishwa daraja kutoka konstebo mpaka koplo.
Alizaliwa kwenye mji wa Nyawa, Tambach Division, wilaya ya Keiyo. Wazazi wake ni Barnaba Kipkoech Korir, mama ni Leah Jepkosgei Kangogo. Caroline ni mtoto wa kwanza kwa wazazi wake, alisoma Shule ya Msingi Nyawa (bweni). Sekondari alisoma shule mbili, alianzia Mtakatifu Francis, Nakuru, kisha Mtakatifu Alphonsus Mutei (shule ya wasichana), iliyopo Kamariny, kwenye mji wa Iten, Keiyo, jimbo la Elgeyo Marakwet.
Mwaka 2008, Caroline alijiunga na Chuo cha Polisi, Kiganjo. Akiwa chuoni hapo, alipata ufaulu wa daraja la kwanza katika ulengaji wa shabaha. Mwaka 2014, alisoma kozi ya ukoplo kwenye Chuo cha Polisi Kenya.
Pamoja na matukio hayo, Caroline ni mke wa ndoa wa Kamishna wa Polisi Kenya, Richard Kipkirui Ngeno. Katika ndoa yao, wana watoto wawili. Kwa jinsi simulizi ya Caroline ilivyo, ni dhahiri hakuwa na maelewano na mume wake. Je, hili sakata la Caroline, Kamishna Ngeno hahusiki?
Ilivyo, ni kama Caroline alikuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa. Msimamo wa Kamishna Ngeno upoje? Kwa nini hawakuwa wakiishi pamoja? Kama waliishi wote, mbona nguo za Konstebo Ogweno zilikutwa chumbani kwa Caroline? Au nguo hizo ziliwekwa kiharamia ili kumuingiza Caroline matatani?
Zipo picha ambazo zimevuja, zinamwonesha Caroline, akitembea barabarani, huku amevaa nguo ambazo ndizo alikutwa kavaa alipokufa. Swali; nani alimpiga picha? Je, alikuwa anafuatiliwa? Na nani? Kwa nini aliyempiga picha hakutoa taarifa ili akamatwe?
Caroline alipokuwa hai, alifanya kazi Chuo cha Polisi Kenya, Mombasa, Kituo cha Polisi Kaloleni, Nakuru, Chuo cha Polisi Kenya, Nakuru, Kituo Kikuu cha Polisi, Nakuru, na mwisho kabisa alihudumia kama polisi wa mahakama (court orderly), Mahakama ya Sheria, Nakuru.
View attachment 2143088