Uchaguzi 2020 Siku 7 kuanza kampeni, wagombea wa CCM mambo bado

nyumbamungu

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2017
Posts
1,033
Reaction score
895
Sina kumbukumbu kama kinachoendelea katika kuchakata majina ya wana CCM waliotangaza niya kugombea Ubunge kama kilishawahi kutokea.

Ilivyozoeleka CCM huwa na kalenda zao ambazo zinatangazwa kabla ya kuanza mchakato wa kugombea nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais lakini awamu hii imekuwa kinyume, kwa kumbukumbu zangu kama nitakuwa sawa mara baada ya kumaliza kuteua wagombea (Urais, Ubunge na Udiwani ) wale waliokosa nafasi huwa wanajiunga na Vyama vya Upinzani.

Kuna kila dalili Uchaguzi 2020, utakuwa wa tofauti kama mtakumbuka CCM walishatangaza mgombea watakaye muacha hataweza kuchukuliwa na Chama chochote, wapo tuliojiuliza itawezekanaje? Kumbe wengine ''Mazoezi" wao "Mechi"

Nimeona katuni ya Kipanya kuna Usafiri upo nje ya jengo lililonakshiwa kwa rangi Njano na Kijani kama inavyojieleza dereva ameitwa achukue abiria kuwapeleka kituo kikuu cha mabasi ( kukata tiketi ya kugombea kwenye chama kingine) yanayosafiri kwenda mkoani, lakini abiria aliyemuita bado hajatoka, dereva amekasirika.... aaghrrrr@#%"*^ huenda anawafokeiya!?!?


NYONGEZA:- Nionavyo ingependaza zaidi kama utaratibu huu wa kupata wagombea ukawekwa kwenye Katiba ya CCM kuondoka sintofahamu kwa wanaogombea na kama itawapendeza zaidi katika kuwataja walioshinda sio vibaya ukawepo muda wa kukata rufaa, hiyo ndio demokrasia na CCM ndio kikongwe vyama vingine vijifunze kutoka kwao.
 
Hakika uchaguzi wa mwaka huu utaleta kumbukumbu isiyomithirika.

Kuna mawaziri, manaibu, DC, RC wakurugenzi wote hao isingekuwa PIN wangetia NIA ila kwa sababu ya PIN wameponea shoka la wajumbe, hivyo wengi wa hao watakuwemo kwenye kinyanganyiro japo hukuona, sikia wakichekechwa na wajumbe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…