FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Well, mimi si mshabiki sana wa soka lakini inanibidi niwe mshabiki kwa kuwa Gozi langu linapenda soka.
Kwa ubishi tu na si kwa ushabiki wa dhati, siku hiyo mimi nilikuwa nawashangilia Ujerumani, Gozi langu linashangilia Brazil. Sikulia kwa kufungwa Brazil, nililia kwa kulionea huruma Gozi langu baada ya goli la tano kumuona akibubujikwa na machozi kwa kichapo walichochezea Brazil, nami nikajikuta ingawa naishangilia Ujerumani lakini machozi yananitoka.
Hii siku nnadhani wengi wengi hawatoisahau ingawa hawataki kuikumbuka.
Last edited by a moderator: