Siku ambayo wapenzi wa soka hawataki kuikumbuka

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,246
Reaction score
123,145

Well, mimi si mshabiki sana wa soka lakini inanibidi niwe mshabiki kwa kuwa Gozi langu linapenda soka.

Kwa ubishi tu na si kwa ushabiki wa dhati, siku hiyo mimi nilikuwa nawashangilia Ujerumani, Gozi langu linashangilia Brazil. Sikulia kwa kufungwa Brazil, nililia kwa kulionea huruma Gozi langu baada ya goli la tano kumuona akibubujikwa na machozi kwa kichapo walichochezea Brazil, nami nikajikuta ingawa naishangilia Ujerumani lakini machozi yananitoka.

Hii siku nnadhani wengi wengi hawatoisahau ingawa hawataki kuikumbuka.
 
Last edited by a moderator:
Uzuri wa huu mchezo kila zama ina historia yake. Na hii ilikua yako na mchepuko wako ila sio kwangu, na wengineo. Mfano mi sintokaa nisahau siku Zizu ana mnyuka kichwa Materez
 
Hahahahaa mimi hua nacheka unavyopenda kusema 'Gozi lako'....
Hiyo siku naikumbuka na nilifurahi sana maana siipendi Brazil.
Nilifurahi sana half ya kwanza ya mchezo Brazuca walipokula 5-0, nilitegemea half ya pili wakoloni wetu wangepiga 5 nyingine ili kukamilisha idadi ya kumi!!!!
Looooh! wakaishia kupata mawili, nadhani wabrazil waliomba wasipigwe nyingi manake kama sio 9 au kumi zilikuwa halali yao.
 
da...nilikuwa na matumaini jamaa watafufuka na kurudi mchezoni lakini wapi bana...hadi zilipo baki dk 5 ndo nikajua kumbe kweli....
 

Wajerumani walitumia ubinadamu tu.Wangeamua kufanya kweli hata dosen wangewapiga.
 
Dah hii siku kweli hata mimi niliumia...! Yani ni kama yule jamaa mnayemtegemea kwa ubaunsa mtaani kwenu aje apigwe na mjamaa mwingine wa mtaa wa pili af kichapo cha mbwa mwizi!

It wasn't pretty!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…