3MMANUEL
Member
- Nov 7, 2012
- 14
- 1
jamani wana jamii naombeni msaada wa kisheria ilikuwa mwezi wa kumi na mbili mwaka 2010 mdogo wangu alifariki dunia baada ya kuchomwa kisu na jambazi na kufanikiwa kunyang'anywa pikipiki,tuliendelea kufanya upelelezi tukafanikiwa kumkamata mtu akitumia ile pikipiki na kumfikisha polisi tangu mwezi wa 2/2011 kila tukifuatilia ile pikipiki mara tunaambiwa yule jamaa aliyekamatwa amemtaja mtu mwingine kuwa ndiye muhusika wa hilo tukio na polisi mbele yetu wamekiri kuwa wameshindwa kumkamata aliyetajwa wakatuomba sisi ndo tuwasaidie kumkamata wakati hatumjui pia wakati mwingine wanatueleza kuwa ofisi yao haina mashine ya photocopy kwa ajili ya kutolea copy zile nyaraka za kesi isitoshe wanataka tuwakabidhi kadi original ya pikipiki.naomba msaada wenu wa kisheria pamoja na ushauri.