Siku hizi vitendo vya rushwa nchini vimekuwa vya kawaida, sijui nani karuhusu hali hii

Siku hizi vitendo vya rushwa nchini vimekuwa vya kawaida, sijui nani karuhusu hali hii

mwanga mweusi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2020
Posts
276
Reaction score
452
Niseme tu kilichopo kuna mradi wa barabara unafanyika huku sisi vijana wa hapa ndio tuliwapokea wachina wakatuajiri kama vibarua, tunalipwa 5000 kwa masaa 10 tumejenga kempu imeisha.

Sasa kinachokasirisha watu wametufukuzwa wakawaita wakenya ndio wakaajiriwa rasmi, hata baadhi yetu waliopo kazini wanalipwa Tsh. 5000 kama vibarua na ndio wanafanya kazi kubwa kuliko wao mshahara wa mwezi uliopita hata kwa wachache walioajiriwa wa hapa hawafiki 5 wamekatwa NSSF ila hawawekewi kwenye akaunti zao na hao wageni wana NSSF na wanalipwa vizuri.

Huu mradi upo Katavi.

Huu uzi niliuandika Agosti 16 ila sikuipost sababu bado nilikua naimani kidogo ila jana Agosti 19 niliyoyaona nikaona niseme tu ya moyoni.

Walikuja watu wa uhamiaji wakawakamata wale wageni wakapigwa pingu nikaona mambo sio mabaya sisi wenyeji tutapata angalau haki zetu. Walienda ofisini wakakaa kama lisaa wakataka wamchukie na huyu mchina aliewaleta wageni kinyemela kilichoendelea huko ofisini nauhakika walipewa pesa [rushwa] wakawaachia wale wageni wakaondoka.

Hii tanzania sio kabisa haki hakuna tena, hela za NSSF za miezi iliyopita watu hawajawekewa na HR anajificha wafanya kazi wakiuliza wajibiwa wamuone HR naye hayupo na wamemwambia asije kazini.

Wanaohusika waangalie na hili jamani.
 
Back
Top Bottom