Siku kama ya leo 2 May,1980 papa John Paul wa Pili aliitembelea Zaire

Siku kama ya leo 2 May,1980 papa John Paul wa Pili aliitembelea Zaire

Basi Nenda

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2017
Posts
20,774
Reaction score
47,866
Leo katika Historia
siku kama ya leo ambayo ilikuwa tarehe 2 May,1980 takribani miaka 40 iliyopita kiongozi mkuu wa kanisa katoriki duniani pope John paul wa pili alifanya Ziara ya kikazi nchini Zaire ambapo alikutana na mwenyeji wake Rais Mobutu Sese Seko
Papa alipokelewa katika mji mkuu wa Kinshasa lakini hata hivo alirudi tena kwa mara ya pili mnamo August 1985 ,Papa huyu alionana mara kadhaa na Rais Mobutu kwani Rais huyo aliwahi kumtembelea Papa huko Vatican
IMG_3277.JPG
IMG_3278.JPG
IMG_3279.JPG
IMG_3280.JPG


NB
Uhusiano wa Mobutu na kanisa katoliki ulikuwa ni wa kusua sua ilianza wakati Mobutu yupo kijana alipewa adhabu na viongozi wa jeshi kwenda jeshini kutokana na kosa lake la kutoroka shuleni ,baada ya hapo Mobutu alichukia kanisa na mambo ya kufunga ndoa lakini Baadae mkewe na kiongozi fulani wa kanisa walifanya kazi kubwa kumrudisha Mobutu Kanisani, lakini baadae tena miaka ya sabini alipiga marufuku kubatiza watoto wa Zaire majina ya kikristo na kutoa adhabu kwa padre yeyote atakayekutwa amembatiza mtoto majina ya dini hiyo mfano John,Yohana nk


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom