Siku kumi na nane hawajaanza kujadili Katiba je tutafanikiwa?

Siku kumi na nane hawajaanza kujadili Katiba je tutafanikiwa?

uswaa

Member
Joined
Mar 4, 2014
Posts
55
Reaction score
20
Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, juzi na jana wamekuwa katika mtihani mgumu wa kufikia uamuzi wa pamoja kuhusu utaratibu wa upigaji kura, kati ya kura ya wazi na kura ya siri.Habari kutoka katika kikao cha ndani cha Chama Cha Mapinduzi (CCM), zilisema kutokana na mvutano huo, mjumbe mmoja, Chritopher Ole Sendeka, alijikuta akilia hadharani akitetea upigaji kura ya wazi.Kikao hicho kilichofanyika juzi kati ya saa 2:00 na saa 5:30 usiku chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kilishuhudia mabishano makali kati ya wanaotaka kura ya siri dhidi ya wale wanaotaka kura ya wazi.Habari hizo zilisema baada ya Pinda kufungua kikao hicho, alimkaribisha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Shamsi Vuai Nahodha, ili atoe mrejesho wa kikao cha mashauriano.Inaelezwa kuwa katika kikao hicho, Nahodha aliwaambia wajumbe kuwa kutokana na mazingira yaliyopo ndani na nje ya Bunge kwa upande mmoja na wananchi kwa upande mwingine, kura ya siri haiepukiki.“Kilio cha Ole Sendeka kwenye party cocaskikao cha chama (party cocus) juzi usiku kilitokana na kauli ya Nahodha kwamba kura ya siri haiepukiki,” alidokeza mbunge mmoja wa CCM aliyehudhuria kikao hicho cha faragha.Mbunge huyo alilidokeza gazeti hili kuwa ndani ya kikao kulikuwa na mabishano makali baada ya kauli ya Nahodha, huku baadhi ya wabunge wakisema wananchi wamechoshwa na msimamo wa CCM.Ni kutokana na mabishano hayo ndipo Ole Sendeka aliposimama akipinga mapendekezo yaliyotaka CCM kulegeza msimamo na kuridhia kura ya siri na wakati alipokuwa akizungumza alipobubujikwa na machozi.Huku akilia katika kikao hicho, inadaiwa Ole Sendeka akisema kwamba kukubali kura ya siri ni kuitosa CCM na msimamo wake wa kutaka muundo wa Serikali mbili.Habari kutoka ndani ya kikao hicho, zilidai kuwa Ole Sendeka alienda mbali zaidi na kusema endapo Pinda ataridhia kura hiyo ya siri, basi yeye (Pinda) na viongozi waandamizi wa CCM waliohudhuria watawajibishwa na CCM.Kutokana na mtafaruku huo, kikao hicho kilishindwa kufikia mwafaka na kuahirishwa hadi jana saa 5:00 asubuhi ambapo hoja ya ama kura ya siri au ya wazi, iliendelea kuwagawa wabunge katikamakundi mawili.Wakati akifungua kikao cha jana, Pinda alisema kutokana na yaliyotokea katika kikao chao cha juzi usiku na baada ya kutafakari kwa mapana yake, chama kimeamua kibakie na msimamo wake wa kura ya wazi.
 
Watanzania hawataacha kukihukumu chama cha Mapinduzi kama kitaacha kubadili msimamo wake wa kura ya wazi. Ni dhahiri kwa wananchi walio wengi kuwa CCM inawacontrol wabunge kwa nguvu badala ya kuacha maamuzi ya hiari kutoka kwao. Kura ikiwa ya wazi tufahamu kuwa itakuwa ni Katiba ya CCM na si ya wananchi wote.
 
Tuende haraka haraka sisi tule waki hii bahati haijirudi kijana acha wazee tule
 
Hv machozi ya ole yana thamani kiasi gani hata kubadili maoni ya watz walio wengi, kimsingi tufahamu kuwa ole kalia machozi mengi sana toka azaliwe na mengi aliyolia hata wazazi wake waliyapuuza, ni wakati muafaka sasa hata chama chake kiyapuuze hayo machozi, alete hoja za kimsingi na si kulialia, na huyo mliaji mwenzake kaogopeshwa na mchozi badala ya hoja, balaaaaa
 
Hv machozi ya ole yana thamani kiasi gani hata kubadili maoni ya watz walio wengi, kimsingi tufahamu kuwa ole kalia machozi mengi sana toka azaliwe na mengi aliyolia hata wazazi wake waliyapuuza, ni wakati muafaka sasa hata chama chake kiyapuuze hayo machozi, alete hoja za kimsingi na si kulialia, na huyo mliaji mwenzake kaogopeshwa na mchozi badala ya hoja, balaaaaa

si afadhali ya machozi ya Pinda ni justifiable.
 
Kwasababu ulaji upo siku zilizopangwa lazima zizidi, watajifanya kuna mambo hawakubaliani nayo wanaganda hapohapo huku siku zinaenda.
Watanzania tuko kimya kabisa, ni kodi zetu hizo jamani.
Mambo yenyewe yanaonyesha tu ulakini wa kupata katiba bora, humo uchama ni mwingi kuanzia tu kanuni za kuendeshea hilo bunge maalumu la katiba.

Hii nchi hii itazidi kulaaniwa sababu wengi ni unafiki tu, nchi zingine watu lazima wahoji kila kinachoenda tofauti, unakuta wanawawajibisha kuanzia raisi mpaka wa chini.
Sisi ni kuangalia tu tunawaachia wanasiasa, wakati nao wana maslahi yao. Ilikuwa sasa tuanze kupaza sauti mambo mengine ya utoto wayafanyayo bungeni ili siku ziende.

Ni upuuzi kuanzisha zogo lisilo na msingi, ili tu bunge lihahirishwe na si mara moja.
Hawatendi haki wakijua hizo posho wachukuazo na watakapoongeza siku kwa makosa yao. Wajue wazi kuna watanzania wenzao wanakufa kwa kukosa huduma za afya, watoto wanakaa chini, hakuna vitabu, wengine shule ina mwalimu mmoja.
 
Hv machozi ya ole yana thamani kiasi gani hata kubadili maoni ya watz walio wengi, kimsingi tufahamu kuwa ole kalia machozi mengi sana toka azaliwe na mengi aliyolia hata wazazi wake waliyapuuza, ni wakati muafaka sasa hata chama chake kiyapuuze hayo machozi, alete hoja za kimsingi na si kulialia, na huyo mliaji mwenzake kaogopeshwa na mchozi badala ya hoja, balaaaaa

Hiki ni kipindi cha watu kuonyesha unafiki wao. Hao wanaolia wanajenga mazingira ya survival kwenye uchaguzi mkuu.

Huyu Sendeka amekuwa siku zote anaipinga Serijali ya CCM. Leo hayo mapenzi ameyatoa wapi? Wache alie tu sisi TUNATAKA KURA YA SIRI,TUNATAKA SERIKALI TATU, TUNATAKA TANGANYIKA YETU.
 
Back
Top Bottom