Zanika
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 1,316
- 752
Dada mange please hid my Idiii (Id)!
Hili limekuwa neno maarufu sana huko insta na kwingine, ambako infomer wa Mange wamekuwa wakimuomba awafiche mara wanapompatia info yoyote iwe ya kweli ama uzushi.
Najiuliza tu Dada yule hana rafiki permanent zaidi ya Maslahi na hii ndio kaliba ya Wamarekani.
Nakumbuka aliyekuwa Balozi wa Marekani wa Tanzania 1998–2001 Balozi Charless Stith, alipokuwa akiaga alitoa Kauli hii "America has no permanent friends or enemies, only interests"
Kauli hii ni maarufu sana tokea miongo ya nyuma ambapo ilinogeshwa na Mwanadiplomasia wa marekani Henry Alfred Kissinger alipochagiza andiko la Dinesh D'Souza:"We have no eternal allies, and we have no perpetual enemies. Our interests are eternal and perpetual" na Kusema "America has no permanent friends or enemies, only interests"
Mara nyingi Mahusiano ya Kimataifa linapokuja suala la maslahi ni ama mataifa yakosane au Yajenge Uhusiano wa Kirafiki, hivyo ndivyo ilivyo pia kwa Wahusika wakubwa na wadogo.
Na ndio sababu Taifa A lililokuwa na uhasama na Taifa B likaondoa tofauti na kuanza/kurudisha uhusiano na hasimu wake. Haya tunayaona sasa hivi ambapo Marekani na China wamekuwa washirika wakubwa kibiashara na kutembeleana kwa ukaribu zaidi tofauti na ilivyokuwa huko nyuma wakati wa miongo ya Mrengo wa Kulia na Kushoto.
Haya pia hutokea kwa watu binafsi ambao aidha kisiasa ama kimahusiano wamekuwa na mitazamo kinzani na kushambuliana kwa hili na lile. Si jambo la kushangaza kuona Member wa Republican akihamia Democratic na kupata Uongozi fulani Kama ambavyo Raisi wa sasa wa Maerekani aliwahi kuwa Mwanachama wa Democratic na baadaye kuhamia Republican ambako ndio ameukwaa Uraisi kwa tiketi ya chama hicho.
Kadhalika hapa kwetu East Africa na hususan Tanzania, kuhama na kubadili mitazamo limekuwa jambo la kawaida kulingana na vile mhusika anavyoona wapi kuna maslahi ya umma(Binafsi???) anayotafuta yatapatikana. Tumeshuhudia wengi wakihama na hata wengine wakitakana radhi na kumaliza tofauti zao na kuponya majeraha waliyopeana wakati uliopita.
Kwa uhalisia Mange Kimambi anajipambanua kuwa ana hasira fulani fulani na amewahi kutafuta nafasi fulani ktk chama cha mapinduzi, jambo ambalo halikuwezekana kutokana na taratibu ambazo yeye ama hakuridhika nazo au hakuzipenda.
Ni wazi kuwa hata awe na nia gani njema ama ovu na apende asipende Tanzania ni kwao na anapapenda na anapahitaji na Hii ndio sababu ya yeye kuwa na hasira na kutumia nguvu yoyote bila kujali anamdhuru nani mradi awe amefikisha ujumbe wake anaoamini ndio suluhisho la yeye kupata anachokitafuta.
Najiuliza Siku akapata yale anayotafuta na ikawa ameyapata kutoka kwa mahasimu wake na kumaliza tofauti zao( Rejea mfano wa China na America pia na Donald Trump). Halafu kwa mnavyomjua ninyi akaamua kuwageuzia kibao wote waliokuwa mstari wa mbele na nyuma.
katika harakati zake. Ni nani watakuwa wa kwanza kuingia mitini na kufuta Id zao? Ama ni nani watahama nchi kwa kuhofia Uzushi waliokuwa wakimpelekea ama ni nani watakimbia/kujisalimisha kwa mipango miovu waliyopanga naye?
ITAKUWAJE NA MTAJIFICHA WAPI??
#GHAFLAANAWAJIBUSIFICHIIDYAMTUMIMI#