realpatriot
Senior Member
- May 28, 2009
- 116
- 76
Heri ya sikukuu ya noeli wadau wote na haswa wana jukwaa,
Najua wengi wetu tumepumzika,napenda kuwapa machache ambayo ukiyaangalia ni kama yana ukweli.
Afrika kama ambavyo mabara mengine huko nyuma kabisa kabla ya ukoloni na kabla ya wanaojiita wastaarabu kuja kwa ajili ya kutufundisha ustaarabu tulikua na maisha ambayo yalipangiliwa katika misingi mbalimbali kwenye kila jambo mfano shughuli zote zilipangiliwa kutokana na jinsia na rika kutokana na jamii husika pia suala la kuomba ama kusali lilifanyika barabara kulingana na jamii husika na mambo yalienda sawasawa.
Tukiangalia kwa undani baadhi ya jamii ambazo kwa asilimia kubwa mpaka leo bado ziko na tamaduni zao na bado kwa asilimia kubwa zinaendele kuabudu miungu yao na kwamba ni kwa kiasi kidogo sana wamechukuliwa na miungu ya magharibi na mashariki wamepiga hatua kubwa za kimaendeleo..
Asia, kwa mfano mpana wao wanaongoza na ukiangalia kuna baadhi ya nchi ambazo zilikua nyuma hata ya zaidi ya baadhi ya nchi barani africa zilikuja zikapita nchi nyingi na sasa ni kinara wa uchumi
Je ni kweli kwamba tungeendela na mila,mungu na tamaduni zetu bila kufuata mungu wa mashariki na mungu wa magharibi tungekua tumepiga hatua kubwa?
Je ni kweli kwamba mila potofu kama kukeketa na zinginezo tungeziacha kadri muda na elimu ambavyo ingeelea kutolewa?
karibuni tuchangie mawazo yetu..ANGALIZO TUWEKE UDINI PEMBENI NA TUJADILI KWA MAPANA