Siku nikifa

mapipando

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
2,922
Reaction score
3,559
Kwanza niwatakie siku njema wakuu.

Nimejaribu kuwaza kwa sauti siku mimi mapipando nitakapo ondoka dunia hii ni nani atajua humu ndani?

Kweli tunafahamiana juu kwa juu,tunataniana, tunapeana like,tunaudhiana,tunachekeshana kweli kiasi kwamba mtu usipoingia humu unajihisi kupungukiwa jambo muhimu.

Kumekuwa na desturi ya kuulizana mbona flani siku hizi haonekani,mbona kimya kimezidi juu ya mchangiaji fulani.Jibu la alipo huyo anaeuliziwa huenda likapatika endapo kuna member mwingine/wengine ambao wanamfahamu/wanafahamiana nje ya jamii forum.

Mbali na Lacute niliyefanikiwa kuonana nae mwaka 2015 ambae hajaonekana mda mrefu humu na pia nimekuwa nikimpigia simu hapatikani,sina ninaemfahamu nje ya hili jukwaa,ndio kusema siku nikifariki jukwaa hili halitajua? halitasikitika kunipoteza? halitanitakia safari njema?

Ni mtazamo tu.
 
Usijali boss njia ni moja hata kama kwenye jukwaa hatutajua
 
kwanza ukifa ubongo utaharibika utapoza every kind of knowledge ulikuwa nayo hapa ulimwenguni...so worry not maana hata kama wakitaka kufufua hutojua hata kuandika, wala ku comment, utakuwa kama zezeta...
usiogope ukifa nothings will be yours tena thus why watu wakifa wanaoza..

kikubwa zaidi ni kuacha historia nzuri kwa ulio waaacha ingawa huko mbele sijui palivyo
 
Sawa,nashukuru japo hiyo haikuwa maana yangu mkuu.
 

RIP Lacute...RIP Mapipando
 
Me nilileta hill wazo LA watubkujuana na kusaidiana katika hizo mambo
Wajuaji wakasema et ,,,,,,,,)
 
Siku ukiugua hebu nipe namba ya ndugu yako wa karibu!! Ukifa atanipa taarifa mkuu!
Mkuu kwann nisikupe sasa hivi maana kuna vifo vingine ni vya ghafla.......!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…