Siku nilipokuwa Mafunzo ya Uaskari Kilimanjaro, Siwezi Msahau Afande Msuya

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Nakumbuka nlikuwa nmemaliza kidato cha nne.baada ya ku browse sana kitaa nikaona bora niwe hata njagu. Basi nikaenda mafunzoni kilimanjaro.

Siku hiyo walikuwa wamepika maharagwe na ugali watu wanaenda kuchukua msosi mi nmesimama pembeni.afande msuya alikuwa anapenda sana kuonekana kwa mademu na sifa.akaja nlipo

"Wewe mbona huendi kuchukua chakula?"
Nikamjibu huku nmegangamaa kidogo baada ya kumpa saluti.maana tulikuwa tumeshaelekezwa namna ya kuheshim wakubwa wetu.

" Nina allergy afande"
Akanitizama na kujibu kwa msisitizo kidogo.

" Hata kama una allergy unatakiwa ule na wenzio chakula cha wote.halafu na hiyo allergy nani amekuruhusu uwe unaitumia hapa? Hapa siyo pikiniki kuwa mje na vyakula vyenu mle huko bwenini.leta hapa hiyo allergy uwagawie hawa wadada hapa nao wale.na nisisikie tena unakuja na allergy kwenye mafunzo utadhani pikiniki."

Hapo nikawa napambana na kuzuia kicheko kiasi koo lilitaka kupasuka.nikajibu tu
"Sawa afande nitafanya hivyo"
 
Akili yako ina sadifu kazi yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenivunja mbavu!!!![emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] ,yaani ulistahili upigwe mitama ya kutosha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…