Wanaweza kushika madaraka kweli hiyo siku ikifika maana ccm kama chama, hakitadumu milele. Muda wake wa kufa ukifika kitakufa tu au kudhoofu na kubakia kuchechemea kama ilivyo kwa chama cha KANU nchini Kenya.
Muhimu wapinzani wakubali kubadilika. mfano wamuandae Rais wao mwenye sifa mapema na si kusubiria yule anayechujwa ccm, kuungana pamoja na kutanguliza maslahi ya nchi badala ya vyama vyao pia ni jambo la muhimu. Kuachana na maisha ya kutegemea tu siasa ili kupunguza wachumia tumbo na wanasiasa vigeugeu, wapiganie mabadiliko ya katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, nk. Kinyume na hapo, itabakia tu kuwa ndoto tena ile ya mchana wapinzani kuja kuingoza hii nchi.