Siku ya Figo Duniani: 7% ya Watanzania wanaathiriwa na Ugonjwa wa Figo

Siku ya Figo Duniani: 7% ya Watanzania wanaathiriwa na Ugonjwa wa Figo

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, 7% ya Watanzania wanaathiriwa na Ugonjwa wa Figo na idadi ya Wagonjwa inaongezeka

Inashauriwa kuzingatia Lishe Bora, kula Matunda/Mbogamboga, kupunguza kiasi cha Chumvi pamoja na Matumizi ya Pombe na Tumbaku

Mtindo wa Maisha na Vyakula tunavyokula vinaweza kuimarisha au kuhatarisha Afya ya Figo

AFYA YA FIGO.jpg

Dalili za Ugonjwa wa Figo
  • Kuvimba uso na macho
  • Kuvimba miguu
  • Kukojoa sana hasa wakati wa usiku
  • Uchovu wa mwili
  • Maumivu ya kifua na kupumua kwa shida
Sababu zinazofanya Mtu kupata Magonjwa ya Figo

1) Kisukari
2) Shinikizo la damu, Saratani
3) Matumizi ya pombe kupita kiasi
4) Magonjwa ya kuambukiza kama Malaria
5) Kuvuta sigara au matumizi ya aina ningine yoyote ya tumbaku
6) Uzito mkubwa kupita kiasi, unene au kitambi
7) Kula vyakula vyenye mafuta, sukari au chumvi kwa wingi

Chanzo: Wizara ya Afya
 
Mfumo mzuri wa kuishi una hitajika Japo Ni swala gumu ila lazima watu tukubali ili kupunguza uwezekano wa kukumbwa na MATATIZO ya kiafya
 
Back
Top Bottom