Siku ya kucheka duniani ....cheka kwa afya yako

MAKULUGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2011
Posts
7,828
Reaction score
10,527
Jumapili ni siku ya kucheka Duniani .....ampapo kila mtu anashauriwa kucheka kwa ajili ya furaha ya moyo wake na amni ya dunia kwa ujumla ,,,,jifunze kucheka uone ni jinsi gani utakuwa na afya bora ....maelezo zaid log on INTERNATIONAL LAUGHTER DAY !KAZI KWAKO
 
Post hii ni nzuri kwani kiafya mtu anayecheka hazeeki mapema.Lakini pia kucheka kuna mahali pake.
 
Waoh,thats wonderful,ngoja nitajitahidi kukaa peke yangu nicheeeke wee,hadi basi?!mtu asiniharibie pozi..ukicheka unarelax hata akili kiukweli,itafanya kazi vizuri,ukinuna au kulia unajiongezea mastress.com
 
Movie za comedy kama 'The gods must be crazy'zinahusu sana!
 
Sherehe zitafanyika wapi kitaifa?
 
@KYALOSANGI

[h=2]Faida na manufaa ya kucheka kwa binadamu[/h]
Manufaa ya kucheka.

Wanasayansi wamekadiria kwamba kucheka kwa furaha kwa nusu dakika ni sawa na kupumzika kabisa kwa dakika 45. Kuangua kicheko kunalingana na kufanya mazoezi ya viungo kwa dakika tatu, hali kutabasanu kwa uchangamfu mara kumi ni sawa na kufanya mazoezi

makali kama ya kuiga makasia kwa kutumia mashini kwa dakika kumi.

Manufaa mengine ya kucheka yanatia ndani kuongezeka mara tatu kwa kiasi cha hewa kinachovutwa ndani ya mapafu na vilevile

kuborashwa kwa mzunguko wa damu, umeng'enyaji, kuyeyushwa kwa chakula, utendaji wa ubongo, na kuondolewa kwa vitu vyenye kudhuru.


"Napendekeza kwamba ili uwe mwenye furaha, jambo la kwanza unalopaswa kufanya kila asubuhi ni kutabasamu na kumwonyesha mwenzi wako na watoto wako tabasamu, kama huna hata jamaa zako.


" Jifunze kUcheka unapokosea, na jaribu kuona mambo kwa njia nzuri hata wakati hali inapokuwa ngumu."


TAFADHALI UNAPOJIFUNZA KUCHEKA UMSICHEKE MZIZIMKAVU ALIYE TOA FAIDA ZA KUCHEKA.
😛oa:focus:

chanzo. https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/226523-faida-na-manufaa-ya-kucheka-kwa-binadamu.html
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…