BARDIZBAH
JF-Expert Member
- Jan 11, 2017
- 5,259
- 10,078
Nimeiiba sehemu.....
Kuna mwanangu baada ya kuchapwa na life, akaamua kujitosa kwenye kazi za saidia fundi.
Kazi ya kwanza aliyokutana nayo kwenye ghorofa moja hapo kariakoo ilikua ni kubeba zege. Kwa jinsi alivyofika tu kazini walivyotizama umbo lake mafundi wakamuambia “Dogo utaweza kweli?” 😂👇
Mwanetu akasema “nitaweza” si unajua shauku na hasira za kuisogelea pesa kivyovyote ile! Mafundi wakasema poa.
Kwa waliofika site za kkoo za maghorofa wanaelewa, fundi yupo ghorofa ya 7 anataka tofali za block zipo floor ya kwanza. Jala la kwanza ikawa kupandisha tofali juu.
Ile kazi mwanetu aliifanya kuanzia saa 2 mpaka mida ya saa sita hivi! Na humo ndani inapigwa mixer ya kubebeshwa makarai ya zege anakimbia nayo pia. Hii sikia tu kwa jirani. Maana kazi ambayo kirahisi ingefanywa na lift inafanywa na binadamu ili kupunguza gharama Za ujenzi 😂
Kufikia saa saba Mchana mwanangu alikua kashasanda kitambo.
Kila akisogeza mguu na karai la zege lipo kichwani anaona hatembei. Hatimae akadondoka na karai chini! Sasa sehemu Za site kunakuaga na wale jamaa wa OSHA (ambao wanasimamia usalama kazini)
Ikabidi mwanangu pale awekwe pembeni kwa sababu alikua kashachoka Ila kusema anashindwa.
Kikasikika kidari kimoja ambacho kilikua kinabeba tofali kikisema “Dogo kashasanda huyu na kwenye mgao hayumo”
Kwa uchungu mkubwa mwanangu alikiri kushindwa moyoni lakini hata hivyo la zaidi zaidi ni jinsi alivyoumizwa na kazi na mwisho wa siku anarudi kapa.
Alinawa miguu kwa huzuni kubwa mno ili asepe! Mara ghafla msimamizi wa vibarua aliyekuepo pembeni akiusoma mchezo wote akasema.
“Usijali Dogo mgao wako utapata” hii ilikua kama sauti kutoka peponi kwani hakuamini na hii ni stori ambayo hatakuja kuisahau maishani mwake.
Kupiga saidia fundi ujipange! Yote kwa yote vijana tusiache kupambana na kujaribu🤝