Siku ya kwanza kutambulishwa ukweni

Candy kisses

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
297
Reaction score
210
Unakumbuka ilikuaje? Unakumbuka ulivaaje?Je walikupokeaje?
Nimeenda na ndugu yangu juzi alikaribishwa ukweni kwa mara ya kwanza....wiki nzima alikua restless,trying to do everything to impress her "inlaws"
tupeane uzoefu,ulijiskiaje baada ya kuondoka??Maana ni kama kufanya interview...loooh!
 
kwa wachaga lazima uende na "usafiri" wa maana. na utoe ofa ya mbege za kutosha kwa shemeji zako+BABA MKWE
 
Duh...

Huko unaenda kama mission fulani hivi.. Unazingatia schedule na topics za kuongea tena ukiwa mtetezi wa mada watakazo kuwa wanapendelea ikibidi hata kusifia mazingira yao

Baada ya hapo unatafuta moments itakayo kusahaulisha hayo madudu yote uliyokuwa ukifanya
 
Wengine tulifumaniwa[emoji30] [emoji30] [emoji30]kila kitu kikamalizwa usiku huo huo kulipambazuka tayari tulikuwa wanadoa
Hiyo kama,mimi nilifumaniwa,ghetto yombo vituka shughuli ikaishia hapo nipo na,mama watoto hadi leo
 
Haya mambo mi bado aisee ngoja nimpate wa kwenda nae kwanza ila inakua kama umemwagiwa maji hata kuongea unasubiri uulizwe kwanza ile kupayuka payuka inapotea kabisa full utii wa maigizo maana hakutakua na uhalisia hata chembe
Ila naamini siku ikitimia nitakua katika uhalisia wangu kabisa
 
Ni kazi wa kuu unaweza kushikwa na tumbo la gesi yaani hapo yule wife sijui utamwona je...

Nashauri hio siku hata upige cha arusha kama puff mbili ndo uzame ukweni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…