Siku ya leo sitaisahau

MstahikiMeya

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2014
Posts
1,633
Reaction score
560
Leo tangu asubuhi nimepiga mishe mishe lakini
zote zimebuma nimejikuta nakosa hadi hela ya
kula mchana
Nikaona ngoja nimpigie simu Jimama wangu
anaitwa Mama Salima ana Mgahawa huku
mtaani ila nilizinguana naye mwezi uliopita
nikaona bora tu nimpigie simu nijipendekeze
niombe msamaha mambo yaishe ili maswala ya
msosi yasiwe yananipa tabu
Nikachukua simu yangu nikampigia maongezi
yakawa hivi
COX.........Halow mambo vipi dear??
Mama Salima........poa upo wewe kijana? Leo
umeamua nini hadi umenipigia simu??
COX........Nimekumisi sana dear wangu yani
tangu tuzinguane sina raha kabisa dear naoma
tuonane tuongee yaishe mpenzi
Mama Salima.......mmmh makubwa mimi nipo
hapa Mgahawani kama unaweza njoo utanikuta
hapa
COX.......Sasa hivi nakuja dear wangu asante kwa
kunipa nafasi ya kuonana na wewe
Mama Salima........usijali we njoo tu utanikuta
hapa
Nimefurahi sana Jimama wangu Mama Salima
alivyonikubalia kuonana naye tena ameniambia
nimfuate Mgahawani nikapanga nikifika cha
kwanza namuambia anipe Wali na kuku nakula
ndo tunaendelea kuongea
Nimeoga fasta fasta nimeingia chumbani kwa
Brother nikavaa suti yake na moka zake ili Mama
Salima akiniona nimeulamba apagawe tena na
mimi
Nimeondoka home kwa mwendo wa kasi sababu
njaa ilikuwa inaniuma sana nikawa nawahi msosi
kabla haujaisha
Nimefika kwenye mgahawa wa Jimama wangu
mama Salima nikamkuta anawahudumia wateja
chakula nikamsalimia nikamuambia na mimi
anipe wali kuku na soda
Mama Salima alivyowahudumia wateja wote
akaniletea wali kuku na soda nikamuambia
"subiri nimalize kula dear ndio tuongee mambo
yetu mwenzio nna njaa sana"
Akaniambia "poa we kula tu mimi nakusubiria"
mama Salima hakujua mimi nimejipendekeza
kwake ili tu anipe wali wa bure
Nimemaliza nikanawa vizuri nikaweka na nne
Mama Salima akaniambia "haya sasa ongea
hicho ulichosema unataka kuniambia"
Nikamuambia "mimi nimekuja kukuomba
turudiane mpenzi mwenzako bado nakupenda
sana nisamehe kwa yote niliyokufanyia mpenzi"
Akanijibu "yani wewe Cox usitegemee kama ipo
siku utakuja tena kurudiana na mimi sahau
kabisa mwanaume gani wewe kila siku kesi hapa
mtaani mara utembee na wanafunzi mara kesi
za uwizi mimi sikuwezi tena unikome uache
kunipigia simu hebu nilipe hela yangu ya chakula
uondoke hapa unanitia kichefu chefu"
Daah nimechanganyikiwa kuona mama Salima
kanibadilikia tena ananidai na hela yake ya
chakula kama 6000 ukicheki mfukoni mimi nna
300 tu
Nikamuambia "sio vizuri mpenzi usinifanyie hivyo
mimi kuishi bila wewe siwezi"
Mama Salima alivyoona naendelea simuelewi
kujitetea akanikunja akaniambia "nipe hela
yangu ya chakula kabla sijakujazia watu hapa"
Nikamuambia "naomba usiniabishe wangu mimi
hapa sina hela nna 300 tu hela yako nitakuletea
kesho" akaniambia "usinitanie na Lichogo lako
hilo hebu nipe hela yangu kumbe unajifanya
unaniomba msamaha turudiane ili ule bure leo
utanitambua"
Mama salima kawaita mama ntilie wenzake
wamenivua koti la suti na moka alafu ukicheki
nilivaa vya brother wamenijazia watu
wamenizomea sana yani nimepata bonge la aibu
nimerudi nyumbani kifua wazi huku niko peku
sijui broo akija nitamuambia nini
Mama Salima kaniumbua sana utafikiri hanijui
kumbe alikuwa Jimama wangu daah nimekoma
 
hahahahahahaha safiiiiiiii nampa big up huyo mama wanawake wote wangekuwa na msimamo kama wake kina yahaya mngeshika adabu
 
cha msingi umekula..

hayo mengine utapata majibu.. si ushashiba boss
 
Naguswa niwape ufadhili (kuwalea) wewe na Mama Salima .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…