Siku ya pili nipo Dar yafuatayo nimejionea

craq

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
859
Reaction score
1,866
Leo ni siku ya pili kuwa jijini Dar na nimekuja kwaajili ya kupata huduma ya matibabu kwenye hospitali ya muhimbili.

Tokea nifike huku dar hio jana nimeshangazwa na hii kitu ase nilikuwa kwenye moja ya daladala ndipo kundi la wanaume wakawa wanapiga stori kusikiliza vizuri kumbe wanahadithiana tamthilia ya sulutani daah bila aibu sijui hadija sultana ana bahati mara yule sijui nani mnoko nk nk

Kiukweli wanaume wa dar hamuonewi haki yenu kusemwa

Sijui nani kawaroga hawa wanaume wenzetu wa dar wanahitaji serious lecture kutoka kwetu wa mikoani maana ni aibu
 
Sasa sisi tutaa Amini vipi hii story yako......!!

Inawezekana umeamua kwenda sambamba na mambo yanavyoenda kuhusu vijana wa Dar!!....
 
Ndo ukaamua uanzishe thread nyiiingi za aina moja? Jf iandae utaratibu wa kushusha watu vyeo.
 
ujinga, maisha ya watu yanakuhusu nini sasa kupangiana namna ya kuishi

fata yaliyokuleta kitendo cha wewe kutuletea huu umbea hapa directly tayari ushakuwa mwanaume wa dar vile vile

acha umama mkuu
 
Inawezkana hata hao pia ni wanaume wa mikoani wametoka huko kuja kufata usululisho huku
 
Wanaume wa dar wakiua panya
 
kwani kuangalia tamthilia ni dhambi? au ni kosa kwa mwanaume?
Yapi yamfahayo mwanaume na yapi yamfahayo mwanamke?
 
Sasa hiyo kitu kama wewe sio mdau umeijuaje?
Yaani usikie watu wanamtaja Hadija basi wewe ukajua ni hiyo kitu unayofikiria? Halafu mwanaume wa mkoani unapata wapi muda wa kuwasikiliza wanaume wenzako wakijadili mambo yao kwenye daladala badala ya kufkkiria jinsi gani utatibiwa magonjwa yako sugu kutoka mkoani?
 
Sibishani na mtu anayesubiri kumwambia rais hana chakula asaidiwe.

Ni safi sana kawakazia. We badala ya kulima umekuja kutibiwa sasa unajitibu ugonjwa wako wa busha halafu unarudi kijijini chakula hauna? Unakufa.
 
wanaume wa mikoani wambeya wambeya sana...

yani dume zima umeskia wanaume wenzako wanapiga story umekuja kuanzisha uzi huku......
 
Sasa ww umejuaje Kama sio mdau was hiyo tamthilia
 
[emoji23] [emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…