Leo ni siku ya pili kuwa jijini Dar na nimekuja kwaajili ya kupata huduma ya matibabu kwenye hospitali ya muhimbili.
Tokea nifike huku dar hio jana nimeshangazwa na hii kitu ase nilikuwa kwenye moja ya daladala ndipo kundi la wanaume wakawa wanapiga stori kusikiliza vizuri kumbe wanahadithiana tamthilia ya sulutani daah bila aibu sijui hadija sultana ana bahati mara yule sijui nani mnoko nk nk
Kiukweli wanaume wa dar hamuonewi haki yenu kusemwa
Sijui nani kawaroga hawa wanaume wenzetu wa dar wanahitaji serious lecture kutoka kwetu wa mikoani maana ni aibu