Siku ya Sheria, Spika wa Bunge na utawala wa sheria

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,325


Jana February 6, 2013 ilikuwa Siku ya Sheria na theme ilikuwa Utawala wa Sheria. Sherehe hizo ambazo ziliongozwa na Rais Jakaya Kikwete zilihudhuriwa na Jaji Mkuu, Mohamed Chade Othman, Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mathias Chikawe, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania Bara, Bw. Francis Stolla na viongozi wengine wa ngazi za juu.

Mmojawapo wa waliohudhuria alikuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Bi. Anne Makinda ambaye pamoja na kufuta hoja zote binafsi za wabunge, amelalamikiwa kukalia rufaa 10 tokea mwaka 2011 bila kuzifanyia maamuzi. Rufaa hizo ni pamoja na ile ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kulitaka Bunge lisitishe uamuzi wa kupewa ujaji wa Mahakama Kuu, jaji mmoja kwa kutokuwa na vigezo vya kuwa na nafasi hiyo kwa mujibu wa Katiba.

Mh. Lissu aliomba mwongozo wa Spika akisema; “Mheshimiwa Spika tunataka utueleze tutaendelea kukata rufaa hadi lini, wakati una rufaa zetu 10 kuanzia mwaka juzi na hujazitolea uamuzi, naomba mwongozo wako Mheshimiwa Spika,” alisema Lissu na kujibiwa na Spika Makinda kuwa, “Rufaa hizo zinafanyiwa kazi na zitatolewa uamuzi.”

Spika analalamikiwa pia kwa kukiuka kanuni kwa makusudi, kiasi cha watu, wakiwemo wabunge, kutaka aondolewe kwenye kiti cha uspika. Spika analalamikiwa kwa kwenda kinyume na 8 ya Bunge inayomtaka Spika na naibu wake watende haki, uadilifu bila chuki kwa wabunge wote.

Pamoja na malalamiko ya kuliendesha bunge bila kufuata kanuni zake, Spika alikuwa kinara kwenye Siku ya Sheria iliyojikita, siku ambayo ilijikita zaidi kwenye Utawala wa Sheria. “Tunapozungumzia Utawala Bora, maana yake kubwa kwa jamii ni kuwepo utawala wa sheria ambao unampa kila mmoja wetu haki yake” siyo tuu mahakamani bali kila mahali ikiwemo bungeni.



Rais Kikwete katika picha ya pamoja na majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Februari 6, 2013



Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na majaji wakuu wastaafu na viongozi wengine Februari 6, 2013.



Rais Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi wa dini pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu Rais wa Mawakili leo. Februari 6, 2013.



Rais Kikwete akisalimiana na Mchungaji Christopher Mtikila leo Februari 6, 2013 katika maadhimisho ya Siku ya Sheria.



Viongozi wa dini ya Kihindu wakielekea kwenye kipaza sauti ili kuomba dua leo Februari 6, 2013 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…