Siku ya tano sasa NACTE wanasema kuna tatizo la mtandao kutoa transcript, nifanyaje?

Siku ya tano sasa NACTE wanasema kuna tatizo la mtandao kutoa transcript, nifanyaje?

CTP

Member
Joined
May 6, 2024
Posts
6
Reaction score
3
Habari zenu ndg Watanzania na wasio Watanzania tulioko humu ndani?

Ndugu zangu awali ya yote poleni na majukumu zaidi shukurani kwa MUUMBA.

Ndungu zangu nipo mbele zenu kwa ombi moja la kuomba ufafanuzi, ushauri juu ya hali anayopitia mdogo wangu hapo ofsi za NACTE Dar, mdogo wangu huyu ni mhitimu miaka kama minne(4) nyuma sasa mdogo wangu huyu kafuata TRANSCRIPT hapo NACTE tarehe 29/04/2024 akajibiwa arudi baada ya May mosi, ndio baada ya may-mosi yaani tarehe 02/05/2024 amerudi pale ofisini kajibiwa kuna TATIZO LA MTANDAO amerudi zaidi ya mala 5 kila akifika anajibiwa mtandao haupo vizuri bado.

Dhumuni la andiko hili ni juu ya hali ya usumbufu anaopitia mdogo wangu,maana katoka mkoani kafikia LODGE kwa muda wote huu na hamna dalili juu ya kupata matokeo yake kumbuka kabla kasafiri chuoni alikosomea wakamwambia taarifa zako zipo vizuri na TRANSCRIPT kuipata nenda NACTE Dar na ndiko alipo ili kukamilisha zoezi hilo. Ajabu ni kwamba toka amefika jibu ni MTANDAO UPO CHINI.

Ndg zangu mdogo wangu huyu kapata ajira ofisi fulani hivi na wanahitaji TRANSCRIPT kukamilisha zoezi baada ya kufaulu INTERVIEW yake. Mdogo wangu huyu amekuwa mpambanaji kwa kujiajiri japo kapitia changamoto nyingi maana kujiajiri ni shughuli kwelikweli, sasa kipindi hiki kapata ajira mahala na ni kama anaenda kukwamishwa na kitu hiki.

Msaada wenu ndg zangu mdogo wangu anaumia hasa ukizingatia PESA ya matumizi LODGE na chakula huko Dar.

Swali najalibu kuwaza hapa hivi kuna shida ya MTANDAO kweli au ni mazingira fulani yanaandaliwa na waliopo ofisini hapo juu ya kijana huyu mtoto wa mkulima na mpambanaji, hivi kweli akose ajira yake kwa mazingira haya. Ndg zangu tusaidiane kunisaidia mdogo wangu huyu.

Mdogo wangu kafikia kukata tamaa PESA nafanya kumtumia maana katumia hadi mtaji wake wote.

MUNGU IBARIKI JF na watu wake ukianza na mwanzilishi wake.

Ahsanteni na sorry kama andiko litaonekana ni refu kusoma.
 
Yaani hata na leo kafika ofisini kajibiwa MTANDAO UPO CHINI, sijui nn afanye tu ili afanyiwe, kweli hakuna mwenye kusaidia katika hili?, Kwamba na hili hadi tuwapigie magoti au kuhusisha viongozi wa juu!, Kama hivyo hakuna mwenye anaweza saidia viongozi hawa kuoneshwa huu usumbufu?,


Endeleeni kutuhamasisha tulipe kodi na kuwa wazalendo katika mazingira haya.
 
Back
Top Bottom