Siku ya Vitabu duniani

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Kaka Francis ahsante kwa kutukumbusha kuhusu Siku ya Vitabu.

Ilikuwa mwaka wa 1957 nina umri wa miaka 5 nimekwenda sokoni na mama yangu Bi. Mwanaidi bint Sheikh Mohamed Mvamila.

Mlango aliopita yeye ni ule wa madrasa na kwa hakika hakuwa anakwenda popote kwa kuwa baba yake ndiye alikuwa mwalimu wa hicho chuo hapo hapo nyumbani kwao.

Mama yangu hakuona mlango wa shule lakini alikuwa mpenzi wa elimu.

Siku moja tumeongozana sokoni hili soko ni soko la Mtaa wa Chini Moshi ndilo lilikuwa soko kubwa kwa miaka ile kabla halijajengwa soko kubwa zaidi Mtaa wa Juu.

Kulikuwa na muuza unga wa mhogo akichanganya na sembe ambao mama yangu akiupenda.

Jirani na muuza unga alikuwapo muuza vitabu.

Mama yangu akaninunulia kitabu cha kujifunza kusoma na mwalimu wa kunishika alif kwa kijiti alikuwa yeye.
Hapo sijaanza hata shule.

Nakikumbuka kitabu kile.

Nasomeshwa, ‘’aeiou, babebibobu,’’ nk. hadi tunafika, ‘’baba kanasa...’’

Naamini wale wa umri wangu watakumbuka haya maneno katika kujifunza kusoma.

Kitabu changu cha kwanza kikubwa kukishika mkononi ingawa nilikuwa siwezi kukisoma sawasawa kilikuwa, ‘’Machimbo ya Mfalme Suleiman’’ cha H. Rider Haggard.

Kitabu hiki kilikuwa cha dada yangu yeye akisoma Girls School shule hii ilikuwa Mtaa wa Kitchwele na Msimbazi na hadi leo shule hii ipo hapo Mtaa wa Uhuru na Msimbazi.

Picha ndani ya kitabu kile zilikamata sana fikra yangu.

Dada yangu alikuwa akija nyumbani na kila aina ya vitabu vingine vya Kiingereza na mimi nikawa nachukua naangalia picha najitahidi kusoma lakini wapi siambulii kitu.

Kitu kingine nikumuusudu dada yangu alikuwa akiimba nyimbo za Kizungu.

Nikawa naona raha kumsikiliza nikajua haya yote kwa kuwa anajua Kiingereza.

Nikawa napenda vitabu na ndiyo maana niliporudi Dar es Salaam likizo kutoka Moshi nilikokuwa nimeanza darasa la kwanza nasoma Lutheran Primary School dada yangu akanipa ‘’Mashimo ya Mfalme Suleiman.’’

Nilisoma Kinondoni Primary School mwaka wa 1963 nikitokea Moshi Majengo Middle School.

Kulikuwa na mwalimu wa Kiingereza Mr. Romenesco.

Huyu alikuja Tanganyika katika mradi wa Peace Corps.

Mr. Romenesco alivyoona bidii yangu katika somo lake akanifanya Mkutubi wa Darasa.

Vitabu vya kusoma mimi ndiyo mwangalizi wa kabati lake.

Hii ilinipa fursa ya kusoma kila kitabu kipya kilicholetwa Dar es Salaam
Tulikuwa na mwalimu wa Kiingereza kutoka Uingereza, Mrs. Grant akisomesha St. Joseph’s Convent.

Mumewe alikuwa Mwalimu Chang’ombe Teacher’s College na yeye kama mkewe akifundisha Kiingereza.

Hawa waliletwa na serikali ya Uingereza kuja kusomesha lugha yao.

Mrs. Grant pia alinipenda na nikawa vilevile Mkutubi wa Darasa.

Hapa ndipo nilipofaidi.

St. Joseph’s ilikuwa shule haina mfanowe kwa uzuri wake katika taalum, masomo na nidhamu.

Mrs. Grant alikuja na ‘’Labaratory,’’ hata sijui niieleze vipi lakini alikuwa anatufundisha kusoma kwa kasi na kuelewa.

Anasimamisha ‘’stop watch’’ yake tunafunga vitabu kisha anauliza maswali.
Nikimaliza na Mrs. Grant nakutana na Ms. Menez mwalimu wa Literature.

Hapa ni William Shakespeare, ‘’The Merchant of Venice,’’ na African Writers Series tunapambana na Chinua Achebe, ‘’Things Fall Apart,’’ na Wole Soyinka, ‘’The Trials of Brother Jero.’’

Ndugu yangu walimu hawa Allah atawalipa kwa hisani waliyonifanyia.

Wanapenda kusomesha na wanasikia raha kusomesha.

Unadhani kumsomesha mtoto wa Kariakoo Kiingereza hadi apate First Class Cambridge Examination ni jambo rahisi?

Ana ulimi mzito kama nanga hicho Kiingereza chenyewe anakiogopa kukisema mbele ya wajuzi wa lugha hiyo katika darasa ambalo kuna wanafunzi Wazungu na Magoa na Waafrika ambao walisoma ‘’special schools,’’ za wakati ule unadhani wewe wa Kinondoni Primary School utafua dafu hapo?

Mrs. Grant ndiye aliyenifanya nijiunge na Tanganyika Library wakati huo ipo Mtaa wa Mkwepu, baadae hii maktaba ikawa ofisi ya Takwimu baada ya kujengwa Maktaba ya Taifa, Titi Street.

Hii Maktaba ilisheheni vitabu.

Hapa ndipo nilipopata wazimu wa vitabu kabisa ambao kwa hakika ulihitaji mganga aniague.

Siku ya Jumatano ni ni nusu siku shule hadi saa saba mwisho.

Nyumbani kwetu ni Libya Street jumba la Posta ya Kisutu.

Nikishakula nabadili nguo nakuja Maktaba hapo Mkwepu.

Vitabu viliyokuwa navipenda ni vile vya ‘’adventure,’’ Spaniards wanakwenda Amerika ya Kusini ndani ya majahazi wanavuka Atlantic Ocean kutokea Spain.

Basi huwezi kuamini akili yangu inahama Dar es Salaam kwa muda naingia katika jahazi na mimi na kuwa baharia na nashiriki katika mikasa yote ambayo mabaharia hawa wanakumbananayo kuanzia dhoruba za baharini hadi kuingia katika visiwa na kufanya vita na wenyeji.

Spaniards wanaingia Aztec na mimi mmoja wa hao askari.

Nikiinua kichwa naangalia nje taa zinawaka Maghrib imeshaingia na mimi niko Dar es Salaam.

Naondoka na vitabu vya kuazima kwenda kusoma nyumbani.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndahani,
Ahsante kaka yangu.
Kuna mtu aliwahi kuniambia ukitaka kutawala dunia lazima uwe unasoma sana. Zamani library zilikuwa zina hazina tele ya kuelimisha kwa wale waliopenda kujisomea.
Siku hizi mambo yamebadilika sana.
 
Kaka Francis ahsante kwa kutukumbusha kuhusu Siku ya Vitabu.

Ilikuwa mwaka wa 1957 nina umri wa miaka 5 nimekwenda sokoni na mama yangu Bi. Mwanaidi bint Sheikh Mohamed Mvamila...

Hongera!

Nadhani hii ni hamasa ya kushea waliotujengea hamasa ya kusoma:

Nitaanza na baba: Yeye alikuwa ananunua magazeti ya NewsWeek na yafananayo nayo. Sijui kusoma Kiingereza, lakini nami nashangaa picha na kuangalia neno mojamoja. Kadhalika alikuwa akinunua LP ("rekodi") za kiingereza, kama vile za Abba Group, zikiwa na maandishi ya nyimbo kwa Kiingereza.

Chekechea ya Police Barracks Kilwa Road (na kwa muda ile ya Ofisi ya TANU Mwananyamala) nilijifunza kusoma na kuandika kwa Kiswahili.

Mama alitununulia kila aina ya vitabu vya hadithi vya Kiswahili. Baadhi ninavyovikumbuka,

1. Paukwa Pakawa. Hiki kilikuwa na hadithi mbalimbali. Natamani nipate nakala. Mojawapo ni kisa cha twiga kuwa na shingo ndefu (hint: mamba anahusika).

2. Musa na Sara. Nakumbuka kipande kisemacho, "nitakuja kula mtama kesho." nadhani sungura alisema.

Maktaba ya nyumbani palikuwa na vitabu vingine vingi vya hadithi, katika miaka iliyofuata.

Shule ya msingi, 1979-80 Mgulani-Chini (siku hizi Barracks), Mwalimu Masamu na wengine waliotufundisha, walitupatia vitabu vingi vya shule. Hadithi ya Hana Hela na Sultani Kipingu, Mwanamalundi na nyinginezo. Mbali na vile vya darasani vyenye hadithi za Heri Mimi Sijasema...

Darasa la tatu na kuendelea Mgulani-Juu palikuwa na mabadiliko makubwa kwenye mfumo wa Elimu. nadhani sisi ndio ilikuwa batch za mwanzo kuanza kutumia vitabu vya Musa na Daudi. Kufika darasa la saba, vitabu vya kina Kalagesye vikiwa vinaishia.

Vitabu vingi vya hadithi za watoto nilivisoma 1979-80 (Darasa la Kwanza na la pili). Kufikia darasa la sita, ndipo nilipoifahamu maktaba ya Tanganyika.

Wakati niko sekondari niliendelea kuitumia. Na nilikuwa napenda kusoma hadithi za "Shanwa". Zilikuwa set mazingira ya Kiafrika na zilikuwa nzuri.

High school, rafiki yangu now Dk. Innocent M., aliniintroduce to Sherlock Holmes. I read all the stories in the books he brought to school.

Thereafter my reading interest has been trying to understand human beings - interesting stuff.

Yeah! Good to know about Siku ya Vitabu Duniani. Asante Mohamed Said kwa mada nzuri.
 
Mlenge,
Unaelekea wewe ni mkali.
Ahsante sana.
 
Kinyungu,
Mmanyema.
Kitu gani kimekufanya wewe kutaka kujua kabila yangu?

Nami kama wewe sina nia mbaya napenda kufahamu tu.
Mkuu navutiwa sana na jinsi ulivyojitolea kuandika historia, mila na desturi za watu wa Dsm hasa hapo katikati kabisa ya jiji. Najua ni wachache sana toma sehemu hiyo waliofanya kazi kubwa kama uliyofanya. Pia naelewa wengi hapo ni wahamiani. Ndiyo maana nimependa kujua asili yako.

Vinginevyo nakupongeza sana kwa kazi zako. Natamani niandike yanayonihusu kama ulivyofanya ww. InshaAllah naomba ndoto yangu itimie.
 
mzee kumbe una miaka 68/69.vipi unafanya mazoezi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Duke...
Kama swali lako ni kuhusu kujua ninavyoishi na athari yake kwa afya yangu hicho ulichouliza si kitu muhimu kwetu.

Athari kubwa ya afya kwetu ni matumizi ya ulevi na uvutaji wa sigara.

Kwa maisha yetu ya kutembea kwa miguu haya na chakula cha shida ni mazoezi tosha.

Ushawaona watu wa kada hii wakienda Gym?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
haya mzee endelea kutupatia historia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waafrika tutaanzisha lini siku ya utumwa(slavery day) kila uchao kuna something day.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…