Mzee wewe ni mpotoshaji namba moja kwanini unaandika ujinga huo
Hao masister wa kikatolic wewe unaandika ujinga kwanini unapotosha mambo Mzee
Wewe hufai kabisa ndani ya jamii ni moja kati ya watu mliopasa kuweko huko Damascus, Allepo au Ghouta mpigwe mabomu ya nguvu huna maana
Masister wakatoliki hao unaleta ujinga na mawazo takataka humu
Gussie,
Kwa kawaida na ndiyo ibra ya historia hii mtu akisoma hasa kwa mara ya kwanza
huwa anapandwa na ghadhabu na mara nyingine hunishabulia hadi kwa matusi.
Nasoma lugha yako hapa ya kughadhibika unatumia neno, ''ujinga,'' unaniita ''mzee.''
Hakika mimi ni mzee na kwangu si tusi wiki mbili zilizopiyanimefikisha miaka 66.
Alhamdulilah na nilikuwa nimesahau kuwa ni siku yangu ya kuzaliwa wanangu ghafla
wakaja na ''suprise,'' ikabidi niwaombe radhi nikimbilie chumbani kubadili nguo maana
keki ilikuwa imebebwa na camera zinanilenga.
Unazungunza kwa hamaki kwa kuingiza mambo ambayo si mada iliyopo mezani hapa.
Unazungumza kuhusu mabomu na mambo ya Allepo nk.
Ikiwa mimi napotosha wewe hukustahili kuja na matusi.
Ungekuja na ukweli ili ufute uongo wangu na hapa wasomaji wangenufauika kwa kujua
ukweli.
Unasema ati nakuja na ''takataka.''
Huu kwangu ni muhali ningekuwa naandika takataka watu wasingejazana hapa jamvini
kunisoma kila wanaponiona nipo.
Punguza ghadhabu na andika kwa adabu ikiwa unataka kufanya mjadala na mimi.
Ninayoandika ni kweli tupu na naweza kukupa ushahidi kwa kila neno langu.