Siku ya wanawake yawa agenda iliyoporwa na mfumo mpya wa kitabaka ndani ya tabaka

bhoke chacha

Member
Joined
Oct 24, 2024
Posts
6
Reaction score
6
SIKU YA WANAWAKE YAWA AGENDA ILIYOPORWA NA MFUMO MPYA WA KITABAKA NDANI YA TABAKA

Ni muhimu kurejesha mwelekeo wa siku hii ili uweze kutumikia lengo lake la awali la kutetea haki za wanawake

Historia ya Siku ya Wanawake

Siku ya Wanawake Duniani ilianza kuadhimishwa rasmi mnamo Machi 8, 1975, baada ya Umoja wa Mataifa kutambua siku hii kama siku rasmi ya kuikumbusha dunia kuhusu haki za wanawake1. Hata hivyo, historia yake inarudi nyuma zaidi, hadi mwaka wa 1908 wakati wanawake 15,000 walipoandamana katika jiji la New York wakidai muda mfupi wa kufanya kazi, malipo bora, na haki ya kupiga kura2.

Mwaka mmoja baadaye, Clara Zetkin alitoa pendekezo la kuanzishwa kwa siku hii katika mkutano wa wafanyakazi wanawake uliofanyika Copenhagen. Pendekezo hili lilipokelewa kwa shangwe na wanawake kutoka nchi 1712. Hivyo basi, Siku ya Wanawake Duniani ilizaliwa kutokana na harakati halisi za wanawake ambao walikuwa wakipigania haki zao

Maana na Malengo

Siku hii ina lengo la kuhamasisha usawa wa kijinsia na kutambua mchango wa wanawake katika jamii. Ni fursa ya kuashiria maendeleo yaliyopatikana lakini pia kuangazia changamoto zinazokabili wanawake duniani kote. Katika muktadha huu, Wadau tuna jukumu muhimu la kuhakikisha kwamba ujumbe wa siku hii unafikia watu wengi na kwamba haki za wanawake zinaendelea kupigiwa debe.

Ushahidi wa Madai ya Kuibwa kwa Siku ya Wanawake

Siku za Usoni siku ya Wanawake imeanza kupata uwelekeo mpya baada ya kuibuka kwa migongano ya kimaslahi miongoni mwa Wanawake .Pamoja na Jamii kusukwa na mifumo ya Kitamaduni,Kisiasa na Kiuchumi hali imekuwa tofauti.

UCHUMI VIJIJINI.

Ushiriki wa wanawake katika shughuli za kiuchumi vijijini ni muhimu sana kwa maendeleo ya jamii na uchumi wa nchi. Ingawa wanawake wanachangia kwa kiasi kikubwa katika sekta ya kilimo na uvuvi, bado wanakabiliwa na changamoto nyingi zinazowakwamisha kufikia usawa wa kijinsia na uwezo wa kiuchumi.

wanawake wanachangia asilimia 34 ya nguvu kazi katika sekta ya kilimo, lakini wanakabiliwa na changamoto kubwa kama vile ukosefu wa ardhi binafsi, upatikanaji mdogo wa mikopo, na ukosefu wa elimu. Hii inawafanya wengi wao kubaki masikini licha ya juhudi zao za kuendeleza familia zao na jamii.

Kwa mfano, ingawa wanaweza kuwa wakulima wazuri, mara nyingi hawapati haki sawa katika kugawana ardhi au kupata mikopo kutoka kwa taasisi za kifedha. Hali hii inawafanya kuwa wategemezi zaidi kwa wanaume katika familia zao, hivyo kupunguza uwezo wao wa kujitegemea.

CHANGAMOTO ILIYOPO.

Pamoja na Mwanamke kuwa muhimili muhimu katika kuchangia ustawi wa Uchumi wa Kaya bado thamani yake huonekana tuu wakati wa Maandalizi ya shamba na Mavuno shambani ,kwenye Jamii nyingi Mwanamke hapeleki mazao Sokoni na kwenye vyama vya Ushirika siyo Mwanamke anaechukuliwa taarifa za akaunti ya Benki ,Jina la akaunti ya benki huchukuliwa la Mwanaume tuu nay eye ndiye huingiziwa fedha.

Hii ni changamoto ambayo unaweza kuidharau lakini kwa baadhi ya Jamii hakuna uwazi juu ya malipo yaliyopatikana kupitia shughuli za uzalishaji wa mali ndani ya ndoa.

Mwanamke wa kijijini amekosa haki ya Jasho lake lakini hii siyo agenda ambayo Wanawake wanaungana kuhakikisha hakuna jasho lisilo na thamani kwenye shughuli za uzalishaji kwenye kaya.
Hoja siyo kusubiri ndoa ivunjike ili mali zinazoonekana zigawanywe. Bali hoja iwe ni shughuli za uzalishaji wa mali za Pamoja kuwe na mfumo wa kudhibiti mfumo kongwe na kujenga mifumo ya uwazi kwenye mapato.

KISIASA.

Mfumo wa kisiasa unaosimikwa katika nchi zetu wa Viti maalumu ,ni mfumo unaotumiwa na Wanawake wenye nguvu wa kuwatumia wanawake wa tabaka la chini kupata Madaraka kutoka kwao kwa dhana ya kuwawakilisha kwenye vyombo vya uamuzi.
Wanawake wanaoingia kwenye mfumo wa Siasa kwa kofia za kundi la Wanawake wanabeba agenda ambazo ndizo mfumo dume ulizibeba toka enzi za ukoloni. Mfumo dume uliokalia viti vya maamuzi ulijadili na kuamua masuala ya elimu,Barabara ,afya na Uchumi pasipo kujadili kwa kina maendeleo kwa mlinganisho wa kijinsia.

Wanawake bado wameingia kwenye vyombo vya maamuzi pasipo kutumia takwimu za elimu kuhusu udahili wa Watoto wa kike shuleni upoje ukilinganisha na rika lengwa lililopo, drop out,ufaulu,miundombinu ya kujifunzia kijinsia ipoje na uwiano wa watumishi kijinsia upoje.

Kuna shule zina waalimu wa kiume watupu ,hii inaathiri ukuaji wa mtoto wa kike shuleni. Kwa hiyo,mfumo wa uwepo wa Wanawake kwenye vyombo vya maamuzi ni mfumo ulioporwa na kuvurugwa kwa maslahi ya tabaka jipya la kitabaka miongoni mwa wanawake.

KWENYE MILA NA DESTURI.
Bado kwenye baadhi ya Jamii mwanamke hawezi kupewa Madaraka ya kuwa msimamizi wa mirathi Pamoja na kusimamia mali za familia. Mila hizi zinashusha hadhi ya ubinadamu na Jitihada za ujenzi wa jamii mpya yenye usawa wa fursa inakuwa haiwezekani. Ujasiri wa Mwanamke unashushwa kuanzia kwenye mifumo ya kijamii.

SIKU YA WANAWAKE IMEPORWA NA SINGLE LADIES KUWATAMBIA WANAUME.
Kundi jipya mjini linalokua kwa kasi kwa sasa ambalo ni Single ladies limepoka Madaraka kutoka kwenye kundi la Wanawake wa Vijijini na wanawake waliokwenye ndoa. Kundi hili limefanikiwa kupora hoja Wanawake na sasa limekuja na hoja mpya ya kujenga uhasama wa kiuhusiano kijinsia na kupoteza malengo.

KUSHINDWA!!!

Msisitizo haupaswi uwe kuwafungia Wanawake peke yao katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto za kijinsia. Ukifanya hivyo hutapata majawabu ya kutosha juu ya kwanini iko hivyo,ilikuwaje,ikoje ,sababu ziko vipi na sasa tunafanyeje.

TUJISAHIHISHE.
Usawa wa Kijinsia siyo Umwanamke!! Hivyo ni muhimu kumrejesha Mwanaumen a Mwanamke kwenye kujadili na kuweka uelekeo mpya wa Usawa wa Kijinsia tuutakao kwa mstakabali wa Maendeleo ya Taifa letu.
 
Kama ulivyo sema mleta mada hii siku imeshaporwa na hao tunaoweza kuwaita single ladies.

Wao kwa sasa vita yao ni dhidi ya mwanaume na sio mfumo , sauti yao ni kubwa kiasi cha kusikika kwangi, ambapo athari za sauti hio inarudi chini kwenye msingi wa maadili na kuufumua ambapo pia hapo mbeleni kidogo tutakuawa na jamii isio na msingi mzuri wa maadili na ndipo taifa litakapo shuhudia athari za moja kwa moja
 
The Abeokuta Women's Revolt (also called the Egba Women's Tax Riot) was a resistance movement led by the Abeokuta Women's Union (AWU) in the late 1940s against the imposition of unfair taxation by the Nigerian colonial government. The women of Abeokuta believed that, under colonialism, their economic roles were declining, while their taxes were increasing.[1] Additionally, they argued that until they were granted representation in local government, they should not be required to pay taxes separately from men. As a result of their protests, four women received seats on the local council, and the taxation of women was ended
============
Chief Funmilayo Ransome-Kuti, MON (/fʊnmi ˈlaɪjoʊ ˈrænsəm ˈkuːti/; born Frances Abigail Olufunmilayo Olufela Folorunso Thomas; 25 October 1900 – 13 April 1978), also known as Funmilayo Aníkúlápó-Kuti, was a Nigerian educator, political campaigner, suffragist, and women's rights activist.👇

 
Also, a good watch on Netflix docuseries by Olasupo Shasore titled:

Jorurney of an African Colony

There is a segment about women's rights and activism in the docuseries. (Ukihitaji kuruka na kutizama kipengele kinacho onyesha uharakati wa Wanawake kutoka Africa) basi...This is featured in the episode titled "Protest & the Women's War"

Source:Wikipedia & Netflix
 
Nimeusoma uzi na nimeupenda niseme tu, Hongereni sana Wanawake kwani bila ninyi maisha sijui yangekuwaje kwakweli.

ila kuna sehemu katika uzi zinazofunika Juhudi za michango ya Wanawake wa Kiafrika. Pamoja.

Kuna vitu vimenisukuma kuongeza mabandiko hapo juu, kutoka maeneo niliyowekea Bold kama inavyo onekana hapo chini;
Na hapa👇
Maswali yaliyoibuka kwangu ni yale yanayowagusa Wasichana wakiwa wakiwatafuta ma role model wao.

Kuna ka usemi "You can't be what you can't see~~ Marian Wright Edelman.

Marian Wright Efelman, is a civil rights activist and founder of the Childrens Defense Fund.

Nonetheless,

Representation(Uwakilishi) matters, empowerment and Inspiration matters.

Je, unafikiri katika uwasilishaji wa hayo maeneo kwenye bold, umewa wakilisha vyema Waafrica?

Je, unafikiri kuna athari zezote hasi au chanya kwa Wasichana wa Kiafrika na
Kitanzania watazipata? Are they going to be Inspired?

Nawasilisha.


Nkaburu
 
Haya ndiyo mawazo ya baadhi ya wanawake

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…