Siku ya wauguzi duniani, 12 May

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412

Mama Frolence Nightingale RIP amekuwa alama muhimu ya uuguzi duniani kutokana na yale aliyoyafanya kwenye hiyo sekta
Tunapoadhimisha siku hii muhimu duniani je Tanzania tuna wauguzi kaliba ya Frolence? Je huduma zetu zikoje kwenye swala zima la afya utabibu na uuguzi?
 
Ukiona hivyo ujue nimeangaza nimewakosa imebidi nichungulie mtaa wa pili[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Nimekusoma...! Naona kwao hakusomeki kabisa naona hata naibu wake kaamua kuwa waziri wa sanaa
 
Ndugu yangu Mshana. Nimekupata Bwashee. Naiheshimu sana TAALUMA ya Uuguzi (Nesing'). Tuwaheshimu. Wanajitoa kwa kazi yao. Maoni yangu ni kuwa WAAJIRI (Serikali na Binafsi) WAJALI sana maslahi na mazingira ya kazi ya Wanesi.... Naomba Mungu azidi kuwabariki katika siku yao hii. Ninaenzi Mchango wa "Dada" Florence. Kauli yake Do the Patient no harm ingehamia kwingine kama: Bungeni, Shuleni/vyuoni, Barabarani (Matrafiki), Mahakamani (Pilatoz na Mawakili), kwenye ardhi, kilimo, mifugo, Tume ya Uchaguzi (Zanzibar na Tanzania), Makanisani, misikitini....na kwingineko.. Dunia ingekuwa ya NEEMA!
Nahavache Mshana...
 
Kuna vitu hatuvipi kipaumbele! Tumebaki kushabikia chura wa snura na ugomvi wa mahusiano binafsi wa kina jide
 
Kuna vitu hatuvipi kipaumbele! Tumebaki kushabikia chura wa snura na ugomvi wa mahusiano binafsi wa kina jide
tunaendeshwa sana na hisia kuliko uhalisia, ukiuliza ishu za akina lugumi zimeishaje hata hatujui, sisi ndo wabongo hakuna wengine kama sisi, ukitaka umbebe mwenzako muwe pamoja ktk mambo ya msingi atakuona unaringa, bora ukomae tu mwenyewe na familia yako..
 
Tatizo tunapenda vitu vya msisimko saana... Yaani vitu vinavyo trend mitandaoni havina mashiko kabisaaa
 
Tatizo tunapenda vitu vya msisimko saana... Yaani vitu vinavyo trend mitandaoni havina mashiko kabisaaa
Mbaya zaidi hii hali imewakumba mpaka viongoziii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…