Siku yako ya kuvisha/kuvishwa Pete ilikuwaje?

Siku yako ya kuvisha/kuvishwa Pete ilikuwaje?

Nrangoo

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2017
Posts
3,407
Reaction score
5,418
Habari wanaJukwaa ..

Nahitaji tupate uzoefu kutoka kwa wale waliotutangulia kwenye hili suala la Engagement.

Wewe na mchumba wako ni mambo gani mlizingatia katika hiyo siku kwa kuanzia na mavazi muonekano n.k kwa kuzingatia na umuhimu wa hiyo siku husika?

Ni mambo gani unahisi ulikosea kuyafanya ,ulitamani kuyafanya , ulikosea kufanya pengine yakakupelekea kupata aibu au ni yapi mazuri ulifanya kwa siku hiyo?

Naomba tupeane vionjo pengine kwa namna mmoja ama nyingine inaweza kumsaidia mmoja wetu wakati akiliendea hilo suala na mwisho wa mwaka huu matukio ya kuvishana Pete na Ndoa ni mengi.

NB:Wale ndugu zetu wa kataa NDOA Uzi hauwahusu huu😃.

Happy Weekend!
 
Unawatonesha watu vidonda vilivyoanza kupona 😹😹

Watu walivalisha Pete mademu zao na tunda wakamegewa ndani ya vitanda vyao.. 🤣
 
Aliniambia nimuvishe pete,nikamwambia mimi si mzungu.Huo ni utamaduni wa wazungu,labda nikupe kishika uchumba kama ilivyo kwenye kabila letu.Story za pete zikaishia hapo.Sasa ni miaka ishirini na watoto watatu juu.Life is good.
 
Hongerw Sana mkuu
 
Kataa ndoa ni wengi aisee. Umewatoa kwenye uzi ila hadi sasa uzi Una comments 9😀😀😀
 
Back
Top Bottom