Siku yangu ya kwanza kujiunga JF nilidhani haya

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
Nakumbuka ilikuwa mwaka 2010 nikiwa natumia ID flani maarufu baadae nikaiacha,

Nilipojiunha JF
1. Nilidhani kila anayetumia jina la mwanamke ni demu kweli, na wengine niliwaibukia nkidhani naweza pata mchumba hapa hapa, haha , na mbaya zaid nikaamini kila mmoja ni mrembo

2. Nilidhani kila anayeleta story MMU ni ya kweli kumbe wengine uchangamsha baraza tu

3.Nilidhani kila mtu anayesema mnyetishaji wangu kasema, nikadhani wana access ikulu ama usalama wa taifa kumbe uongo mtupu

4. Nilidhani kila anayesema niko ulaya yupo kweli kumbe wengine ni story but wanasimuliwa wanatuletea,

5. Mbaya zaid nilidhani ........

Je we ulipojiunga JF siku ya kwanza ulikuwa na mawazo gani?
 
Nachofahamu Mimi watu tulip wakorofi humu na tunaocoment sana in real life tuko very Introvert na Watu wasiochangia sana ndio Extrovert hatari in real life (waongeaji kupitiliza)

Mbaya zaidi, ogopa wale wanaojifanya sana hekima au wanashauri washenzi hao bora sisi mambumbumbu.
 
Kumbe ilo nalo laweza kuwa kweli waweza kutupatia mfano??
 
Were muhaya nawewe ile kashfa yako ya kutapeli watu humu jf kwenda ulaya tukuweke wapi?
Unataka twende ulaya kumbe we uko BK aka British Kingdom (Bukoba) unakula ndizi za kusongwa na senene
 
Nilidhani wana jf wote wana digrii kumbe wengine wa digidigi[emoji38][emoji38]
Mbaya zaidi nikadhani wote wana magari na mabiashara makubwa darisalamu

Siku hizi nasikia asilimia 79.7% ya wana jf wanakunywa beer za Eagle[emoji125][emoji125][emoji125]
 
Were muhaya nawewe ile kashfa yako ya kutapeli watu humu jf kwenda ulaya tukuweke wapi?
Unataka twende ulaya kumbe we uko BK aka British Kingdom (Bukoba) unakula ndizi za kusongwa na senene
Hahaha we wasema
 
Nilidhani wana jf wote wana digrii kumbe wengine wa digidigi[emoji38][emoji38]
Mbaya zaidi nikadhani wote wana magari na mabiashara makubwa darisalamu

Siku hizi nasikia asilimia 79.7% ya wana jf wanakunywa beer za Eagle[emoji125][emoji125][emoji125]
Wengine wana degree za hotel management za pale amazon
 
Mwaka 2010, wakati natumia ACC ya brother, nilidhani ili ujiunge JF unatakiwa uwe na shahada moja kama yeye, lakini nikazamia na ka form four kangu, na natamba nako πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…