Siku za kocha Pablo wa Simba zaanza kuhesabika

Mmadiridi mwenye tikitaka yake imekuaje tena jamani mbona mapema sana?

Mwacheni atupe tikitaka.
Siyo kila mfumo unafanya kazi kila mahali. Hata ukimleta Klopp anaweza kufeli.

Simba inahitaji usajili wa maana Tena mkubwa.

Kagere, Bocco, Mugalu, Bwallya siwaoni wakiwa na msaada Tena KWA Simba.

Kanoute ni mzuri akicheza na Mkude. Lkn sioni km ataisaidia sana timu huko tuendako..

Pengo la Tadeo Lwanga linaonekana wazi.

Simba km timu inahitaji kufanya jambo kubwa mwisho wa msimu KWA kufanya usajili wa watu wa maana. Naona wanahitaji kuisuka timu upya.
 
Ameishafukuzwa tayari

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Tatizo la Simba siyo kocha, ni ujuha wa Simba kutosajili wachezaji (hasa washambuliaji) wa maana kwenye dirisha kubwa na hili dogo lililofungwa hivi karibuni.

Kwa hawa akina Mugala,Bocco,Kagere,n.k kocha Da Rossa mlimuonea bure,na huyu Pablo mnataka kumwonea,hata Juggen Klopp au Pep Guadiola mnaofikiria kuwaleta nao mtawafukuza tu.
 
Kwani Pablo hakuona?maana alikuwepo wakati wa dirisha dogo
 
Ni kweli mkuu- mm pia naamini tatizo sio kocha- tatizo ni usajili na mipango mibovu- kwa nini kwa mfano hawa -kusajili kiungo mkabaji mwingine ili asaidiane na Lwanga- mm Napendekeza ni bora kocha angejaribu kumchezesha Inonga Kama kiungo mkabaji, nyuma abaki Wawa na Onyango- zaidi ya hapo tusubirie nwakani- uza Bocco, mzamiru, Mgalu, Kagere, Bwalya, Dilunga, Nyoni, Morrison, leta vifaa vipya
 
Hakuna wa kuyanunua hayo makapi
 
Hakuna wa kuyanunua hayo makapi
Ni makapi kwa humu mtandaoni, lkn ktk mpira wote hao watasajiliwa haraka sana KWA timu zetu. Kwamba Ruvu, Prison, Geita hawamhitaji Kagere au Dilunga , au Morisson.

Kuna wakati ushabiki ukizidi utajikuta umedumaa akili.

Kuna wakati mm japo ni shabiki wa Simba, lkn huwa naongea ukweli kuhusu Simba hata km ni ukweli unaoumiza. Mfano sasa hivi nimefikia hatua nakiri Simba haiko vizuri.
 
Unamlaumu vipi Pablo wakati wachezaji wanapata nafasi 6 za wazi wanashindwa kufunga.. Mnataka aingie acheze?
 
kwani Pablo kipindi cha usajili hakuwepo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…