Siku za mwizi 20 check hii

charger

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2010
Posts
2,320
Reaction score
1,371
Jamaa ana mpenziwe wamependa kiukweli wanavodai wao nakuelezana hivyo kiasi kwamba,password za bank card,e-mail wamepeana.Wameahidiana hawatakuja kusalitiana milele.

Wote hawa wana ujuzi kutumia mitandao ya kijamii kama huu.Wote wapo kwenye mtandao fulani na siku ya siku wakajikuta wanachati kwenye thread na mara Ku PM each other wakitumia majina yao ya bandia.Na kila mmoja asijue anachat na nani hasa.Ikafika point wakakubaliana kuwa wapenzi kwani walikua wanaambiana hawana wapenzi wengine.

Mambo yakaendelea hivi kule home wakirudi kila mtu akijifanya mtakatifu kwa mwenzie na kuonyeshana mapenzi motomoto wala hathubutu kutaja mchumba mpya wa kwenye mtandao.

Basi huko mtandaoni wakati wakichat wakakubaliana kwamba imefika muda sasa wakutane na kufahamiana zaidi.Mwanaume kampa location mwanamke kwamba akae hapo taxi itakuja kumchukua na kumpeleka hotel na chumba alipo.Siku haikukawia ikafika dada kachukuliwa kama ilivyo pangwa kupelekwa huko kwa mpenzi.Gari imefika Hotelini dada kapelekwa kaonyeshwa chumba,kagonga mlango,mlango ukafunguliwa......................guess what happened!!!!!alafu uniambie hii kesi itapelekwa mahakama gani?
 
tukio kama hilo,litawasaidia kuimarisha ndoa yao.maana nani atamlaumu mwenzie?na wote wakosaji.litawafanya wajifunze,huko walikotaka kwenda hakuna faida yoyote ile
 
Kaka nashukuru kwa hadisi nzuuuuuuuuuuuuuri kabla sijaenda kulala.
Nadhani wana MMU wenzangu tutakuwa tumeburudika. Haya tumwombe Invisible azime taa tukalale, kesho asubuhi kuwajibika
Gnite
 
Kama msichana ntasema nilijua tu toka mwanzo unanisaliti mpenzi wangu ndo maana nimekuja mpaka hapa kukukamata namgeuzia zali jamaa:wink2::wink2::wink2::wink2:
 
Kama msichana ntasema nilijua tu toka mwanzo unanisaliti mpenzi wangu ndo maana nimekuja mpaka hapa kukukamata namgeuzia zali jamaa:wink2::wink2::wink2::wink2:

na mimi nakujibu, nilijua tu mpenz wangu unanidanganya, ndio maana nakaamua kufuatilia nyendo zako mpaka leo hii nimekudaka red handed,,, sasa sjui nani ataonekana mkweli hapa
 
tatizo wanawake w cku hz vicheche sana ....ht km 2mefumaniani mwanamke lazima nimtie vibao.
 
tatizo wanawake w cku hz vicheche sana ....ht km 2mefumaniani mwanamke lazima nimtie vibao.

Duuu mkubwa, wote vicheche halafu umpige mwenzako.... byu the way hadithi nzuri sana kwa kulalia!!!!!!
 
imekaa vizuri japo najaribu kupata picha hali kama hii ikitokea mziki wake unakuaje,je mnakuwa kama mmemwagiwa maji au mtaanza kurushiana maneno
 
Asiye na dhambi na awe wa kwanza kumpiga jiwe mwenzie kwa hao wahusika.
 
Duuu mkubwa, wote vicheche halafu umpige mwenzako.... byu the way hadithi nzuri sana kwa kulalia!!!!!!

dah! huo wako uonevu.. kwenye cheni bandia kwa hela feki, m1 hufaidika zaidi. Kwa hapa nini?
 
Kama msichana ntasema nilijua tu toka mwanzo unanisaliti mpenzi wangu ndo maana nimekuja mpaka hapa kukukamata namgeuzia zali jamaa:wink2::wink2::wink2::wink2:

Yani hapa umesema, nakauka kama vile sio mimi yani, halafu naanza kumbe ndo zako, kwa nini lakini?
 
Huyu sister na yeye kazidi. Yaani first meeting Chumbani?
 
Huyu sister na yeye kazidi. Yaani first meeting Chumbani?

Sasa tatizo unasahau kuwa ameolewa kwa hiyo meeting isipokuwa chumbani anaweza kuonekana na kuzua maswali- kumbuka Chumbani kuna privacy ya kutosha.

By the way ingekuwa mimi ningemwambia tu-do tuu kwa vile venue nshalipia. Halafu nahakikisha style za cku hiyo zinakuwa za ukweli zaidi!
 
Kama nimimi namchechia kumbe ndiyo tabia yako ndivyo huwa unanifanyia cku zote akiri namchapa nao kisha namsamehe tunalisongesha najua atakuwa amejifunza
 
ina maana hawakupeana number za simu? hata meeting waliarrange throgh mtandao?
 
Yaani hapo ni kubadili kibao tu nilikuwa nakuona tu kwenye laptop unavyochat na mimi nikajiunga ili nikukamate ha ha ha hiyo ni kali sana
 
na mimi nakujibu, nilijua tu mpenz wangu unanidanganya, ndio maana nakaamua kufuatilia nyendo zako mpaka leo hii nimekudaka red handed,,, sasa sjui nani ataonekana mkweli hapa

Kama msichana ntasema nilijua tu toka mwanzo unanisaliti mpenzi wangu ndo maana nimekuja mpaka hapa kukukamata namgeuzia zali jamaa:wink2::wink2::wink2::wink2:

Nyote mtaonekana mafisadi wakubwa, mnakwepa kama anavyokwepa Rostama Aziza umiliki wa Du - Hanz
 
Kwa mtazamo wa ghafla huu ni uongo. Yaani hata mtu hujui anaonekanaje, hamjawahi kuonana, braki ya kwanza ndani ya gest????!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…