Siku zingerudi nyuma ningebadilisha masomo niliyosoma

TAI DUME

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2014
Posts
9,748
Reaction score
26,238
Wakuu nimezaliwa na kukulia mwambao wa ziwa nyasa.
Leo nimetafakari sana mstakabali wa profesheno niliyonayo, hakika haitasaidia taifa langu hata kidogo. Hapa ninawaza, kwa kuwa shuguli kuu ya wakazi wa mwambao wa ziwa nyasa ni uvuvi mdogo mdogo usio na tija,
  • vipi kama serikali ingetuwekea shule au chuo cha uvuvi,
  • ingetupa maarifa kuhusu uvuvi wenye manufaa,
  • ingetuwekea mitaala mizuri ya jinsi ya ufugaji wa samaki ktk mabwawa ili kuendeleza uzalishaji,
  • ingetujengea viwanda au kutufundisha utaalamu jinsi ya kusindika samaki kwa ajili ya soko la ndani na la nje,
  • Ingetuwekea masharti nafuu katika kununua au kukodi vyombo bora vya uvuv. Naona kabisa leo hii watu wa mwambao tungekuwa exporters wakubwa wa samaki nje ya nchi na pia tungekuwa walipa kodi wazuri kwa serikali yetu. Anywei labda mwanangu atayakuta mazingira haya ambayo mimi niliyakosa. Rasilimali tunazo ila raia wanazidi kuwa masikini. Naipenda nchi yangu
 
Tatizo sio kusoma ama kuvua. Tatizo utapata capital ya vifaa vya uvuvi?

Kwanza Serikali yenyewe haitaki ndio maana wakaua hata viwanda. Serikali inataka na inafurahi Mhindi aje hapa awekeze wao wawe wanaenda kuchukua tu rushwa basi.

Hawajali hata kama huyo Mhindi akijaze kiwanda ndugu zake kutoka India
 

inaumiza sana kwakweli
 
Wahenga walisema elimu haina mwisho
Hivyo muda bado unao ndugu
 
Wengi wetu tunafanya ndoto za wazazi ama jamii na si ndoto zetu.

Tuhakikishe watoto wetu hayawakuti haya.

Ila ndugu usisomee kazi,wenyewe wanasemaga success follows excelency.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…