Siku zote nataka kujua ukomunisti ilikuwa ni Imani iliyoamini katika nini hasa

Siku zote nataka kujua ukomunisti ilikuwa ni Imani iliyoamini katika nini hasa

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
10,356
Reaction score
16,379
karne ya 20 inakumbukwa hasa kwa dhuluma za kidini zisizowahi kutokea: hasa Ukomunisti, ulioteka Urusi ukaenea polepole hadi kutawala theluthi moja ya binadamu wote, ulipiga vita dini kwa namna zote na kuua mamilioni ya waamini, hasa Waorthodoksi.

Hatimaye, chini ya Papa Yohane Paulo II, wa kwanza kutoka mataifa ya Kislavi, Wapolandi walifaulu kuangusha serikali ya Kikomunisti, wakifuata na wenzao wa nchi zote za Ulaya Mashariki.

Baada ya hapo, Ukristo uliamka upya katika nchi hizo.
 
Ukomunist haukotokea urusi, urusi ni mtekelezaji tu, myahudi aliyezaliwa ujerumani anayeitwa Karl Marx ndo aliyeandika theory za u-komunist Karne ya 19, na hii na baada ya yeye kuuchukia ubepari (capitalism), kwa urus alikua anatekeleza kile alichoandika Karl max
 
IGWE kaa ukijua Comunist inayojieleza kwa watu ni tofaut na uhalisia
Alaf ata sijazungumzia ubepari Mimi
Ila Juma kila moja ale kwa jasho lake
Trust me communist is blood of all evils in modern daya
 
Jirani anamiliki ng'ombe. Serikali inamchukua huyo ng'ombe, alafu inatugawia maziwa sisi na jirani yetu sawasawa!
 
ukomunisti ni ubepari, uliokakaa kwenye mgongo wa watawala, ndio maana mwananchi wanakuwa hawana vitu vya kifahari eg magari, tv,,internet ,safari za nje kutanua, simu, vinywaji vitamu etc wao kazi zao ngumu tu, lakini watawala wanakula bata
mfano north Korea, kipindi cha nyerere
 
Ukomunisti na ubepari ni ndugu wa baba na mama mmoja
Mifumo yote hiyo Haina hata chembe ya usawa
 
JUKWAA LA WAJAMAA TANZANIA (JULAWATA)

Lengo la Jukwaa hili ni kuendeleza nadharia na mapambano ya kudai Ujamaa na Umajumui wa Afrika. Siku zote, na popote tunapokuwa, tunasimama upande wa wavujajasho. Tunaupinga ubepari katika sura zake zote (ubeberu, uliberali mamboleo, n.k ) pamoja na mifumo mingine kandamizi inayostawisha ubepari (mfumo dume, ubaguzi wa rangi, ukabila, udini, ukaburu wa kiumri, n.k ). Tunapambana kuibomoa mifumo hii yote ili kujenga mifumo inayozingatia uhuru, utu, haki na, usawa.
karne ya 20 inakumbukwa hasa kwa dhuluma za kidini zisizowahi kutokea: hasa Ukomunisti, ulioteka Urusi ukaenea polepole hadi kutawala theluthi moja ya binadamu wote, ulipiga vita dini kwa namna zote na kuua mamilioni ya waamini, hasa Waorthodoksi.

Hatimaye, chini ya Papa Yohane Paulo II, wa kwanza kutoka mataifa ya Kislavi, Wapolandi walifaulu kuangusha serikali ya Kikomunisti, wakifuata na wenzao wa nchi zote za Ulaya Mashariki.

Baada ya hapo, Ukristo uliamka upya katika nchi hizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom