Sikubaliani na kauli za Kibaguzi za kisiasa za MO.

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Kwa kauli yangu na akili yangu ilivyo na usawia wake sikupendezwa kabisa na kauli za kisiasa za Mo kwenye Tamasha letu la Simba Day. Kauli ambazo hazikubaliki michezoni na zinalenga kutugawa wanasimba na zaidi kabisa kutuaminisha kuwa klabu yetu inatumika zaidi kwa manufaa ya kisiasa kuliko kutumia kwa lengo la kuburudisha wana simba kwa ujumla wake.

Kauli kama zile zinaenenda kinyume kabisa na sheria na kanuni za FIFA & IFAB kwa ujumla. Ipo sababu ya kumdhibiti mtu huyu ama ikiwezekana awekewe watu wa mpira karibu yake ili waweze kumpa soma limpasalo kuhusu soka. Sitaki aje kutuharibia hapo baadaye.

"Huyu Mtu Jamani Adhibitiwe"
 
Mo jana alikua high sana alichanganya tambuu na ugoro nadhani ni msongo wa mawazo wa zile billion 20 alizoshindwa kuweka kwenye account ya club.
 
Kwani kasemaje naomba sauti ya Mwamedi
 
Mo jana alikua high sana alichanganya tambuu na ugoro nadhani ni msongo wa mawazo wa zile billion 20 alizoshindwa kuweka kwenye account ya club.

Inasikitisha sana aisee. Yawezekana huyu Boss wetu anahitajika kuonana na Madaktari wa afya ya akili mapema iwezekanavyo. Kama hatakuwa na tatiuzo lolote lile la akili basi huenda kuna pahala anatupeleka na simba yetu ambako ata sisi wenyewe wanachama hatupatambui hakika.
 
Simba na Yanga wote ni CCM piga uwa.misingi ya kuanzishwa kwa Yanga imetokana na Tanu kwa sasa ni CCM
Baadhi ya viongozi wa Yanga wakati huo walijiengua wakaanzisha timu yao ya sunderland ambayo ndo Simba ya sasa.
ni lazima cheche za siasa zitakuwemo kwenye hizi timu mbili na hasa ukizingatia hiki ni kipindi cha kampeni.na sisi watanzania tuna hulka ya kuchanganya siasa kwenye kundi kubwa la watu kama dini,mpira n,k
 
Simba na yanga ni timu za chama na zinatumika kisiasa siku zote, na huko nyuma zilitumika kwenye harakati za uhuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…