Wakusoma 12
JF-Expert Member
- Jul 3, 2017
- 4,035
- 11,462
Wakuu amani iwe nanyi.
Hivi Jana tarehe 10 Februari waziri wa kilimo prof Mkenda alitoa msimamo wa Serikali juu ya sharehe za maonesho ya kilimo ya wakulima Nanenane, ambapo alisema kuwa serikali imeamua kufutilia mbali sherehe hizo.
Moja ya sababu kuu aliyotoa kiongozi huyo ni pamoja na kuelekeza pesa zilizotengwa katika uandaaji na ufanikishaji wa maonesho hayo katika shughuri zingine. Mimi binafsi napinga kufutwa kwa sherehe hizo kwa sababu zifuatazo.
1. Nanenane huadhimishwa kama sehemu ya kuutambua mchango wa kilimo na wakulima kwa ujumla katika ukuaji wa uchumi wa taifa letu, hivyo kufuta sherehe hizi ni kupuuza suala mhimu sana ambalo ndilo linapaswa kusisitizwa katika kipindi hiki cha ukosefu wa ajira kwa vijana wengi.
2. Maonesho ya Nanenane yanaenda sanjari na maonesho mbalimbali ya teknolojia za kilimo hivyo kuyafuta ni sawa na kudidimiza sekta ya viwanda kupitia sekta zake ndogondogo kama SIDO.
3. Maonesho ya Nanenane huenda pia na matangazo ya biashara mbalimbali za mazao hivyo kuzifuta ni kuwanyima wakulima haki ya kutangaza bidhaa zao za kilimo.
Hivyo naiomba Wizara husika ijaribu kukifikiria suala hili kwa uwazi zaidi ili kukinusuru kilimo chetu na biashara zetu.
# kilimo ni biashara.